Nyumba hizo zilizokuwa katika Kitalu namba 314
chenye mgogoro wa umiliki, zilikuwa zinajengwa na John kwa kasi bila
kujali kuwa kulikuwa na amri ya Baraza la Ardhi ya kuzuia ujenzi huo
hadi mgogoro uliohusu eneo hilo utakapotatuliwa.
Wakati wa ubomoaji huo uliosimamiwa na Manispaa ya
Kinondoni chini ya Mhandisi Baraka Mkuya, kulikuwa na ulinzi mkali wa
polisi wenye bunduki na mabomu ya machozi, wakiongozwa na Ofisa wa
Operesheni, Emmanuel Tille.
Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Alphayo Kidata alisema
kuwa ametoa agizo hilo kwa sababu sheria zinapaswa kuzingatiwa na
kwamba nyumba hizo zilijengwa bila kuwa na kibali chochote cha manispaa
kama inavyotakiwa.
“Kuwapo kwa kesi mahakamani hakuzuii sheria nyingine kutekelezwa, wamejenga hawana kibali,” alisema Kidata.
Wakili wa John, Emmanuel Augustino alidai kwamba hatua hiyo imetekelezwa kibabe na katibu mkuu, kwa kuwa kuna kesi wamefungua katika Baraza la Ardhi Kinondoni ambayo inaendelea kusikilizwa.
Wakili wa John, Emmanuel Augustino alidai kwamba hatua hiyo imetekelezwa kibabe na katibu mkuu, kwa kuwa kuna kesi wamefungua katika Baraza la Ardhi Kinondoni ambayo inaendelea kusikilizwa.
“Anajua wazi kuwa alichokifanya ni kinyume cha sheria, ameingilia uhuru wa mahakama,” alisema.
Augustino alisema hawajui watamshtaki nani ili
kudai fidia, hasa kwa kuwa katibu mkuu alitoa agizo la mdomo na hakuna
barua yoyote aliyoandika ambayo ingeweza kutumika kama ushahidi.
Wakili wa anayedaiwa kuwa mmiliki wa kiwanja hicho
cha Janet Kiwia, ambaye ni Howard Msechu kutoka katika Kampuni ya
Uwakili ya Homac, alisema wamefurahishwa na hatua hiyo kwa sababu
walikiuka amri ya Baraza la Ardhi ya kupiga marufuku shughuli za ujenzi
kuendelea.
0 comments:
Post a Comment