Alisema mbali na sifa hizo, Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (Nec) inatakiwa kusimamia uchaguzi huo kwa haki na kuhakikisha
kuwa daftari la kudumu la wapiga kura linafanyiwa maboresho ili kila
Mtanzania apige kura kwa mujibu wa Katiba.
Sumaye alisema hayo jana wakati wa uzinduzi wa
albamu Rose Muhando iitwayo ‘Kamata Pindo la Yesu’ katika Ukumbi wa
Diamond Jubilee.
Alisema sifa ya kwanza ni kuwa na kiongozi
anayetambua, kuulinda na kuthamini umoja... “Kiongozi tunayemtaka lazima
atambue hilo na awe tayari kuchukua hatua za kutuimarisha kuwa na nguvu
zaidi za kiuchumi na kuimarisha muungano wetu na baadaye muungano wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki na hatimaye Afrika.”
Alisema sifa ya pili, kiongozi lazima awe wa watu
wote na anayejiamini kwa maelezo kuwa mtu wa aina hiyo anakuwa na uelewa
thabiti wa kujua matatizo na matarajio ya anaotaka kuwaongoza.
“Sifa ya tatu ni uadilifu, kiongozi mwadilifu ni
yule ambaye hupenda kutenda haki na kuhakikisha anaowaongoza wanatenda
na wanatendewa haki ipasavyo kutoka kwa wote wanaotakiwa kutoa hizo
haki.
Alitaja sifa ya nne kuwa kiongozi anayepiga vita
rushwa na maovu mengine kama ufisadi, matumizi ya dawa za kulevya,
mauaji na ujambazi na asiwe mfanyabiashara.
“Hivi mtu akiingia Ikulu kwa kununua wapiga kura
akifika huko kazi yake ya kwanza itakuwa nini? Kwa vyovyote atarudisha
kwanza fedha alizowahonga na atafanya hivyo kwa kupokea rushwa kutoka
kwa matajiri wanaotaka huduma au mali za nchi yetu,” alisema.
Alisema sifa ya tano ni awe kiongozi atakayepiga vita umaskini kwa kuweka mipango thabiti ya kusimamia rasilimali za nchi. “Kiongozi tunayemtaka lazima awe na uwezo wa kuwa na serikali inayoweza kujadiliana na wawekezaji ili rasilimali zetu ziwanufaishe na Watanzania.”
Alisema sifa ya tano ni awe kiongozi atakayepiga vita umaskini kwa kuweka mipango thabiti ya kusimamia rasilimali za nchi. “Kiongozi tunayemtaka lazima awe na uwezo wa kuwa na serikali inayoweza kujadiliana na wawekezaji ili rasilimali zetu ziwanufaishe na Watanzania.”
Alisema sifa ya sita ni kiongozi atakayeweza
kuboresha huduma za jamii kutokana na nchi hivi sasa kuwa na utaratibu
usioridhisha wa upatikanaji wa huduma za afya, hasa kwa wajawazito na
watoto.
“Saba, tunahitaji kiongozi mwenye nidhamu na
utendaji wake wa kazi. Kuna tatizo kubwa la kushuka kwa nidhamu katika
kazi hasa sekta ya umma na kusababisha shughuli ndogo kufanywa kwa muda
mrefu. Hali hii inafanya sekta nyingi kudorora,” alisema.
Kwa Habari Zaidi Bofya na Endelea........
0 comments:
Post a Comment