Washiriki wa semina wakiwemo maafisa wa TMF na Wanahabari Mkoa wa Mbeya wakifuatilia kwa makini
BAADHI
ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya wametoa duku duku lao kwa Mfuko wa
vyombo vya habari nchini(TMF) kuhusu utaratibu wa kupata ruzuku kwa
ajili ya kufanya kazi za uchunguzi.
Malalamiko
hayo yalitolewa jana mbele ya viongozi wa TMF katika semina
iliyofanyika katika ukumbi wa GR Hotel iliyopo Soweto jijini Mbeya
ambapo waandishi wa Habari walipata fursa ya kutoa ya moyoni.
Awali
Afisa Ruzuku wa TMF, Japhet Sanga, katika utangulizi wake aliuliza
idadi ya waandishi waliowahi kunufaika na Mfuko huo kwa Mkoa mzima tangu
uanzishwe ambapo waandishi sita waliweza kujitokeza.
Kutokana
na idadi hizo Afisa huyo alizidi kuhoji ni kwanini idadi iwe ndogo
kiasi hicho ukilinganisha na utitili wa Waandishi wa Habari uliopo Mkoa
wa Mbeya.
Wakichangia
hoja baadhi ya waandishi walisema wanahisi kuwepo kwa hali ya upendeleo
kwa baadhi ya waandishi kujirudia kupata ruzuku aidha kwa kuangalia
majina ama kupata chochote kutoka kwa mwandishi(ten percent).
Hata
hivyo changamoto nyingi zilizozungumzwa na Wanahabari, Afisa Ruzuku
alisema zimechukuliwa na kufanyiwa kazi kisha kuendelea na ufafanuzi juu
ya namna ya kuomba ruzuku kwa kufuata vigezo na masharti.
0 comments:
Post a Comment