Kenya imekata rufaa ya marufuku ya kocha Adel Amrouche
Kenya imekata rufaa ya marufuku
ya mwaka mmoja iliyopewa kocha wa timu ya taifa Adel Amrouche na
shirikisho la soka barani Afrika CAF.
Amrouche alipigwa marufuku hiyo baada ya kudaiwa
kumtemea mate afisa msimamizi wa mechi baina ya Harambee Stars ya Kenya
na Comoros mwezi Mei.
katibu wa Shirikisho la soka la
Kenya FKF Michael Esakwa ameiambia BBC kuwa tayari wameshatuma ombi la
kukata rufaa kwa shirikisho la CAF .
Kenya imekata rufaa ya marufuku ya kocha Adel Amrouche
"baada ya kuona video ya tukio hilo linalodaiwa kutokea baada ya mechi nina hakika kuwa hakuna aliyetemewa mate ''.
Sadfa ni kuwa kocha mkuu wa Comoros Amir Abdou
amepuzilia mbali uwezekano wa tukio hilo akisema haiwezekani kuwa
Amrouche alimtemea mate afisa huyo.
''Mimi mwenyewe nili kuwepo na pia nilitazama
video na kwa hakika ninaunga mkono FKF maanake hii ilikuwa ni mechi
ambayo tulishiriki.''
Ujumbe huo wa kocha Abdou ulimpiga jeki Esakwa
ambaye anasema kuwa taarifa hiyo itakuwa kati ya habari
watakazopendekeza kutumiwa katika rufaa hiyo.
Kenya imekata rufaa ya marufuku ya kocha Adel Amrouche
Kufuatia marufuku hiyo ya Amrouche, Kenyasasa
inamtegemea Kocha mbadala James Nandwa kuiongoza Kenya katika mechi ya
mkondo wa pili ya kufuzu kwa mechi ya kuwania kufuzu kwa dimba la
mabingwa wa Afrika dhidi ya Lesotho.
Mechi hiyo itachezwa wikiendi hii mjini Nairobi.
Kenya ilishindwa katika mkondo wa kwanza kwa bao moja kwa nunge ugenini.
0 comments:
Post a Comment