Picha ya Maktaba ikimwonyesha mgonjwa wa Congo mwenye umri wa miaka 43 akiwa kituo cha wagonjwa wa Ebola Septemba 29,2007
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imesema
watu wawili wamekufa kutokana na ugonjwa wa Ebola, uliolipuka
kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo.
Hao ni wagonjwa wa kwanza wa Ebola kuripotiwa
nje ya Afrika Magharibi tangu kuzuka kwa ugonjwa huo huko, ingawaje
haijaeleweka wazi kama vifo vya watu hao vinahusiana na mlipuko wa Ebola
katika nchi za Afrika Magharibi.
Mpaka sasa watu 1,427 wamekufa kutokana na maambukizo ya virusi vya Ebola.
Shirika la Afya Duniani, WHO limesema kasi na kiwango cha milipuko hiyo hakijawahi kutokea hapo kabla.
Watu wanaokadiriwa kufikia 2,615 Afrika Magharibi wameambukizwa ugonjwa wa Ebola tangu uzuke mwezi Machi mwaka huu.
Hakuna tiba inayojulikana kutibu ugonjwa huu
lakini baadhi ya watu walioambukizwa virusi vya Ebola wamepata nafuu
baada ya kupewa dawa ya Zmapp iliyo katika majaribio.
Hata hivyo dawa hiyo imeadimika kwa sasa.
Hata hivyo dawa hiyo imeadimika kwa sasa.
Pia Jumapili, mfanyakazi wa afya wa Uingereza
aliambukizwa ugonjwa wa Ebola nchini Sierra Leone na kurejeshwa
Uingereza akisafirishwa na ndege ya jeshi la Uingereza, RAF.
Ni mgonjwa wa kwanza Mwingereza kuthibitishwa kuambukizwa virusi vya Ebola wakati wa mlipuko wa sasa wa ugonjwa huo.
Ni mgonjwa wa kwanza Mwingereza kuthibitishwa kuambukizwa virusi vya Ebola wakati wa mlipuko wa sasa wa ugonjwa huo.
Marekani imetuma vifaa vya tiba kusaidia kupambana na mlipuko wa Ebola nchini Liberia.
Watu kadha wamekufa katika kipindi cha mwezi
uliopita baada ya kuugua homa isiyojulikana katika jimbo la Equateur
katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Jumapili, Waziri wa Afya wa DR Congo Felix
Kabange Numbi amesema watu wawili kati ya wanane waliopimwa ugonjwa
Ebola wamethibitika kuambukizwa ugonjwa huo.
Ameiambia BBC kuwa eneo la karantini litawekwa
katika eneo la kipenyo cha kilomita za mraba 100 katika eneo la Boende
ambao wagonjwa wamegundulika.
Amesema huu ni mlipuko wa saba wa ugonjwa wa Ebola nchini DR Congo.
Virusi vya ugonjwa wa Ebola kwa mara ya kwanza viligundulika nchini humo mwaka 1976 karibu na Mto Ebola.
Bwana Numbi amesema vipimo zaidi vinafanyika.
Jumamosi, bunge la Sierra Leone lilipitisha sheria mpya kuwa ni kosa la jinai kuwaficha wagonjwa wa Ebola.
Tayari watu zaidi wamekufa katika mlipuko huu wa
Ebola kuliko milipuko mingine iliyowahi kutokea. Kama sheria hiyo
itaidhinishwa na rais, wale wanaokamatwa kwa kuwaficha wagonjwa
watakabiliwa na adhabu ya kifungo jela cha kufikia miaka miwili.
Hatua hii imekuja baada ya Ivory Coast kufunga mipaka yake ya nchi ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa Ebola nchini humo.
Nchi hiyo tayari imepiga marufuku safari za ndege kwenda na kutoka Sierra Leone, Liberia na Guinea.
Gabon, Senegal, Cameroon na Afrika Kusini zimechukua hatua kama hizo.
Shirika la Afya Duniani linasema upigaji
marufuku safari za ndege hakusaidii, na kinachotakiwa ni madaktari zaidi
na maafisa kusaidia kuwafuatilia walioambukizwa Ebola, ikiwa ni pamoja
na kuwa na maabara zaidi za kuhama.
Wiki iliyopita, madaktari wawili wa Marekani
waliruhusiwa kutoka hospitalini nchini Liberia baada ya kupewa dawa ya
ZMapp drug, wakati ambapo madaktari watatu wa Liberia pia wanaendelea
vema.
Ugonjwa wa Ebola unaenezwa kati ya binadamu kwa
kugusana moja kwa moja na majimaji ya mtu aliyeambukizwa ugonjwa huo. Ni
moja kati ya magonjwa hatari kuliko yote duniani, ambapo asilimia 90 ya
watu wanaoambukizwa ugonjwa wa Ebola hufariki dunia.
0 comments:
Post a Comment