
Mkurugenzi
wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),
Crescentius Magori akizungumza na Wachezaji wa Timu ya Yanga wakati wa
mkutano wao wa kuzungumzia umuhimu kwa wachezaji hao kumiliki nyumba
zao,uliofanyika leo kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Kitengo cha Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la
Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume akifafanua jambo mbele ya
wachezaji wa timu ya Yanga na viongozi wa timu hiyo (hawapo pichani)
wakati wa mkutano huo uliofanyika leo kwenye hoteli ya Serena jijini Dar
es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Timu ya Yanga,Beno Njovu akieleza nia ya Timu yake ya kutaka
kuwawezesha wachezaji wao waweze kuwa na Nyumba zao wenyewe.
Watendaji wakuu wa NSSF
Sehemu ya Uongozi wa Timu ya Yanga chini ya Kocha Mkuu,Marcio Maximo.
Wachezaji wa Yanga wakipitia vipeperushi walivyopewa juu mradi wa nyumba za bei nafuu za NSSF.
Baadhi ya Wachezaji wa Yanga wakifatilia kwa makini maelezo waliyokuwa wakipewa.
******
KLABU ya yanga imeingia makubaliano ya kununua nyumba kwa ajili ya wachezaji wake na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) .
Akizungumza
jijini Dar es Salaam leo katika mkutano maalum na wachezaji hao
Mkurugenzi wa uendeshaji NSSF, Crescentius Magori amewaambia wachezaji
hao kuwa "kijana mjanja mjini ni yule ambaye ana miliki nyumba ama ardhi
kuliko magari" huku akiwahamasisha wachezaji wa Yanga kuchangamkia
ununuzi wa nyumba hizo ambazo ziko katika mradi wa makao mapya katika
kijiji cha Dege Kigamboni jijini
Dar es Salaam.
“Sisi
tuko tayari kuwapa fomu na kwenda kuwaonyesha nyumba hizo ambazo
zimejengwa kisasa zaidi hivyo ningependa kuwashauri pindi mnapopata
fedha zenu za mikataba mkitoa kiasi ili kuweza kuwa kati ya wamiliki wa
nyumba hizo” alisema Magori.
“Endapo
utaweza kumudu na kutoa kiasi cha sh. mil.8 taslimu na kulipa kwa miezi
mitatu mfululizo unapewa NSSF wanamupa funguo na kuendelea kulipa kila
mwisho wa mwezi hadi kwa miaka 15 unakuwa mmiliki halali wa nyumba
hiyo”alisema Magori.
Aidha
aliongeza kwa kuwaambia wachezaji hao kwamba endapo utakufa ndugu
anaweza kurithi nyumba hiyo. Huku akiwasisitiza wachezaji ambao bado
hawajajiunga na NSSF kufanya hivyo mara moja ili waweze kujivunia
matunda ya uchezaji wa mpira hapo baadaye.
Wakati
huohuo Katibu wa Yanga Beno Njovu aliwaambia waandishi wa habari kwamba
hayo ni mawazo ya Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji ambaye alizungumza
na Mkurugenzi wa NSSF Ramadhan Dau ambapo wote kwa pamoja wameamua
kuwawezesha wachezaji wa timu hiyo ili waweze kuwa na mali zao za kudumu
hadi uzeeni.
0 comments:
Post a Comment