Kwa
haraka unaweza usiamini macho yako na hata ukibidi unaweza kuomba maji
unawe uso ili uweze kuyaamini macho yako kile kinachoonekana mbele yako
kama hivi.
Lakini
baada ya kuamini macho yako bado unaweza kubaki na maswali mengi yasiyo
na majibu, kwamba ni miujiza, Kiini macho au ni nini, na kubwa zaidi ni
jinsi gani binti huyu anayeonekana kuwa ni mrefu kwa umbo amewezaje
kuingia ndani ya Sanduku hili la Chips na kuenea na kuweza kujikunja
kama hivi na kisha kuuchapa usingizi mnono bila shaka???.
Kiukweli
unaweza kuwa eneo la tukio kwa muda wote hadi unaondoka na ukawa bado
hujapata jibu la kujiridhisha na hasa unapokuwa ukisikia la kila mtu
akisema yake kuhusiana na tukio hilo na ndivyo ilivyotokea juzi usiku
huko eneo la Yombo jijini Dar es Salaam, ambapo Binti huyu alikutwa
akiwa ameuchapa usingizi mzito ndani ya Sanduku lenye Chips na Mishikaki
kibao.
Haikuweza
kufahamika kwa haraka undani wa tukio hili. WADAU HIZI CHIPS
HIZIIIIIII, KUWENI MACHO MTAJA KULA MISHIKAKI KUMBE NI YA JIMTU KAMA
HUYU. Picha kwa hisani ya Mtaa kwa Mtaa.
0 comments:
Post a Comment