SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, July 23, 2014

Benki ya Exim Tanzania yaandaa futari kwa wateja wake wa mkoani Tanga

 Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Suleiman Lighuchu akizungumza wakati wa futari iliyoandaliwa na Benki ya Exim Tanzania kwa wateja wake wa mkoani Tanga hivi karibuni. Wa pili kushoto ni Meneja wa Benki ya Exim Tawi la Tanga, Deogratius Makwaia, Mgeni Rasmi Meya wa Jiji la Tanga, Mhe. Omary Uledi (Wa pili kulia)na Katibu wa Bakwata wa Mkoa, Bw. Mohamed Riami (wa kwanza kulia).
 Meya wa Jiji la Tanga, Mhe. Omary Uledi, ambaye pia ni mgeni rasmi (wapili kulia)  akizungumza wakati wa futari iliyoandaliwa na Benki ya Exim Tanzania kwa wateja wake wa mkoani Tanga hivi karibuni. Wa pili kushoto ni Meneja wa Benki ya Exim Tawi la Tanga, Deogratius Makwaia, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Suleiman Lighuchu (watatu kushoto)na Katibu wa Bakwata wa Mkoa, Bw. Mohamed Riami (wa kwanza kulia)
 Baadhi ya wateja wa Benki ya Exim Tanzania na wafanyakazi wakifuatilia yaliyokuwa yakizungumzwa wakati wa futari iliyoandaliwa na benki hiyo mkoani Tanga kwa ajili ya wateja wake.
Baadhi ya wateja wa Benki ya Exim Tanzania na wafanyakazi wakichukua vyakula mbali mbali vilivyoandaliwa malum kwa ajili ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo mkoani Tanga kwa ajili ya wateja wake. 

0 comments:

Post a Comment