SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, June 30, 2014

RATIBA YA RAMADHAN LEICESTER UK

Assalaamu Alaykum,
Jumuia ya Kiislamu ya An Noor ya Leicester Uingereza inapenda kuwatakia
Waislamu wote mfungo mwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Allah akujaalieni nyote afya na nguvu za kutekeleza ibada nyingi zaidi ndani Ya Mwezi huu Adhimu. Pia awape Shufaa ndugu zetu wenye matatizo ya Kiafya na mengineyo. Amin

Jumuia ya An Noor inapenda pia kuwatangazia Waislamu wenzao waishio Leicester Na vitongoji vya karibu kuwa Programu ya Ramadhan InshaaAllah
Itaendelea kama kawaida mwaka huu kwa utaratibu wa Kawaida.
Kila Jumamosi na Jumapili kutakuwa na Darasa za Mwezi wa Ramadhan
Kuanzia Saa Moja na Nusu jioni katika jengo letu 170a Belgrave Gate LE1 3XL Leicester
Baada ya hapo tutakuwa na Futari ya pamoja.
Kama kawaida kila Familia itashiriki katika kuleta futari
Kadhalika kila Familia inakumbushwa kuchangia £5 kila wiki kwa ajili ya Maandalizi.
Programu InshaaAllah itaanza Jumamosi 5/7/2014.
Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na hawa wafuatao:

Malik 07983614261 au ust Farid 07792174408
au tutumie 
email: madrasatulnoor.01@gmail.com
Kullu Am Wa Antum Bikhayr


Mohammed Omar, 
Mwenyekiti wa Jumuia