Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi akiongea na wadau mbalimbali wa elimu wa mkoa wa Dar es salaam wakiwemo walimu wa shule za msingi na sekondari,wamiliki wa shule binafsi na wanafunzi wakati wa hafla ya Siku ya Elimu mkoani Dar es salaam leo.Katika hafla hiyo washindi wa mitihani ya taifa kwa mwaka 2013 kutoka shule za msingi na sekondari za serikali na binafsi wametunukiwa vyeti na zawadi mbalimbali kutokana na ufanisi wao katika utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).
Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Raymond Mapunda akiongea na wadau mbalimbali wa elimu wa mkoa wa Dar es salaam wakiwemo walimu wa shule za msingi na sekondari,wamiliki wa shule binafsi na wanafunzi wakati wa hafla ya Siku ya Elimu mkoani Dar es salaam.
Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za jijini Dar es salaam waliohudhuria hafla ya Siku ya Elimu mkoa wa Dar Es Salaam wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea wakati wa hafla hiyo.
Wadau wa elimu wakiwemo wazazi, walimu wa shule za sekondari na msingi, wamiliki wa shule binafsi na viongozi mbalimbali wakishangilia mafanikio na ushindi wa mkoa wa Dar es salaam katika mitihani ya taifa ya shule za Msingi na Sekondari kwa mwaka 2013 leo jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya Siku ya Elimu.
Mkurugenzi wa Shule ya shule ya Sekondari ya Tusiime ya jijini Dar es salaam Bw. Albert Katagira akipokea cheti cha ushindi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Raymond Mushi (kulia) kufuatia shule yake kutoa wanafunzi bora katika ufaulu wa masomo katika mitihani ya taifa kwa ngazi ya taifa na mkoa wa Dar es salaam kwa shule binafsi.
Mwalimu Stella Kasheba (kulia) kutoka shule ya Sekondari Zanaki akipokea cheti cha ushindi kwa niaba ya Mkuu wa shule hiyo kufuatia shule ya Sekondari Zanaki ya jijini Dar es salaam kutoa mshindi Bora wa Jumla kwa shule za sekondari za serikali katika mitihani ya taifa kwa mwaka 2013.
Mwanafunzi Hussein Hemed Hussein wa Shule ya Msingi Tusiime akipokea cheti cha pongezi kwa kuwa mshindi Bora wa jumla katika mitihani ya Taifa kwa mwaka 2013 kwa shule za Binafsi za jiji la Dar es salaam.
Mwanafunzi Hussein Hemed Hussein wa Shule ya Msingi Tusiime akionesha cheti cha pongezi kwa kuwa mshindi Bora wa jumla kwa wavulana katika mitihani ya Taifa kwa mwaka 2013 kwa shule za Binafsi za jiji la Dar es salaam alichokabidhiwa na Mkuu wa wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi katika hafla ya Siku ya Elimu jijini Dar es salaam.
Mwanafunzi Joyce Lymo wa Shule ya Sekondari Kanosa, Kinondoni akionesha cheti cha pongezi kwa kuwa mshindi Bora wa jumla kwa wasichana katika mitihani ya Taifa kwa mwaka 2013 alichokabidhiwa na Mkuu wa wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi katika hafla ya Siku ya Elimu jijini Dar es salaam.
Wadau wa elimu wakiwemo wazazi, walimu wa shule za sekondari na msingi, wamiliki wa shule binafsi na viongozi mbalimbali wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa hafla ya Siku ya Elimu mkoa wa Dar es salaam.
Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.