Mvua kubwa zilizonyesha zimesababisha mafuriko na madhara makubwa. Juhudi za uokoji zinaendelea siku ya pili Kaskazini mashariki mwa Afghanistan ambapo watu wapatao elfu mbili wanasadikiwa kufa kutokana na maporomoko ya ardhi katika maeneo ya vijiji kwenye mkoa wa Badakhshan.
Vijiji hivyo vimefunikwa na udongo wenye ukubwa wa karibu mita
kumi kwenda juu baada ya sehem ya mlima mmoja kuporomoja kutokana na mvua kubwa
zinazonyesha.
Miili ya watu wapata 350 imepatikana hapo jana
katika maporomoko ya ardhi kazkazini mashariki mwa taifa hilo na hakuna mtu
yoyote aliyepatikana akiwa hai.Umoja wa Mataifa unasema karibu watu 4000 hawana
makazi.
Mashirika ya misaada na uokoaji kwa sasa
wameanza kuwapa mikate na maji maelfu ya watu waliolala nje kwenye baridi kali
wakiwa hawana makazi.
Kuna taarifa nyingine zinazosema maelfu mengine ya watu huenda
wakawa wametoweka baada ya upande mmoja wa mlima kuangukia kijiji k katika eneo
la mashambani la mkoa wa Badakhshan unaopakana na mataifa ya Tajikistan,Uchina
na pakistan.
Waokoaji
wamekuwa wakilalamika kuwa hawana vifaa vya kutosha kuwasaka manusura.
Mwandishi
wa BBC mjini kabul anasema kuwa eneo hilo ni miongoni mwa maeneo yenye umaskini
mkubwa na katika taifa maskini duniani na huenda ikachukua majuma kadhaa kabla
ya serikali kubaini ukubwa wa janga hilo.
HABARI NA BBC SWAHILI
PICHA NA YAHOO