SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, May 5, 2014

MTAALAMU WA NYASI BANDIA KUTOKA FIFA DR.IAN McCLEMENTS ATUA BUKOBA, APIMA UWANJA WA KAITABA LEO

Na Faustine Ruta, Bukoba
Mtaalamu wa nyasi bandia kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Ian McClements amewasili Bukoba leo hii Asubuhi kwa Ndege ya kukodi. 
McClements akiwa hapa Bukoba amekagua Uwanja wa Kaitaba, na baadae amekwea tena ndege yake kuelekea  jijini Mwanza kukagua Uwanja wa Nyamagana.
Dr. Ian McClements akiteta jambo na Jumanne Chama Umande ambaye ni Katibu wa KRFA kwenye Uwanja wa Kaitaba leo hii.
Viwanja hivi vinawekwa nyasi bandia kwa ufadhili wa FIFA chini ya mpango wa misaada wa Goal Projects. Baada ya ukaguzi huo, McClements atatuma ripoti yake FIFA ili shirikisho hilo liweze kuteua mkandarasi wa kufanya kazi hiyo.
Kwa Tanzania viwanja vilivyowekwa nyasi bandia hadi sasa kupitia Goal Project ni Uwanja wa Uhuru uliopo Dar es Salaam, Uwanja wa Karume (Dar es Salaam) na Uwanja wa Gombani uliopo Pemba.
Dr. Ian McClements (kulia) akipata maelekezo kutoka kwa Eng. George Geofrey wa Manispaa hapa Bukoba
Dr. Ian McClementsNje kidogo ya mipaka ya Uwanja Dr. Ian McClements analazimika kuchimba ili aweze kuona chini kuna nini? akitaka kupima maji yanafyonzwa vipi na ni udongo gani? na Je Maji yananyonywa vipi na udongo wa hapa Kaitaba ususani kwenye uwanja huu huu wanaotaka kuuwekea nyasi za Bandia.
Dr. Ian McClements jembe mkononi.
Kumbe kuna mchanga chini, yes! safi
Dr. Ian McClements akichimba chini ili kupima na kuona udogo upi ulipo chini, Amehimba katika maeneo matatu tofauti tofauti na kubaini tofauti.
Dr. Ian McClements (kulia) akichukua kumbukumbu kushoto ni Eng. George Geofrey wa Manispaa hapa Bukoba.
Dr. Ian McClement akipima kina
Dr. Ian McClement alimwaga maji ndani ya shimo ili kuona kaji nini kitafata na je yatanyonywa na udongo kwa muda gani!
Ili chukua muda wa dakika 1 na sekunde 40 tu maji yalikuwa yameishatowekaAkipima maji aliyoweka
Kumbukumbu zikichukuliwa na Dr. Ian McClement kwenye uwanja wa Kaitaba, kumbuka atatuma ripoti yake FIFA ili shirikisho hilo liweze kuteua mkandarasi wa kufanya kazi hiyo.
Dr. Ian McClements akichukua maelezo kutoka kwa Eng. George Geofrey wa Manispaa hapa Bukoba
Alichima na sehemu ya upande wa pili wa goli
Dr. Ian McClements akiteta jambo na Kiongozi Katibu wa KRFA Jumanne Chama
Hapa mchanga hakuna na Udongo wake ni Mweusi mchanga upo chini zaidi
Dr. Ian McClements baada ya kumaliza kazi yake alipaa kuelekea jijini Mwanza na hapa alikuwa anaagana na Jumanne Chama kwenye Uwanja wa Ndege
Mwewe yupo tayari!