Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa rsami na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ndugu Ahmed Kipozi mara baada ya kuwasili kwenye Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mandera iliyoko wilayani Pagamoyo tarehe 10.5.2014.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mandera Ndugu Rose Ummy akisalimiana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati alipowasili kwenye shule hiyo tarehe 10.5.2014.
Mke wa Rais na Mlezi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mandera akisalimiana na baadhi ya walimu wa Shule hiyo mara alipowasili shuleni hapo kwa ziara ya siku moja tarehe 10.5.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongozana na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mandera Ndugu Rose Ummy (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ndugu Ahmed Kipozi (kulia) na wageni wengine wakitembelea maeneo mbalimbali ya shule hiyo.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatilia jaribio la somo la Fizikia (Hooke’s Law: Inayosema ‘The force needed to extend or compress a spring by some distance is proportional to that distance’) lililokuwa likifanywa na mwanafunzi Mwajuma Mwanankuta wa Kidato cha 4 katika Shule ya Sekondari ya wasichana ya Mandera tarehe 10.5.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ya saluti ya Girl Guides kutoka shule ya sekondari ya wasichana ya Mandera .
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mandera iliyoko Wilayani Bagamoyo wakiimba wimbo wa shule kwa ajili ya kumkariisha Mlezi wa shule hiyo Mama Salma Kikwete alipotembelea shule hiyo tarehe 10.5.2014.
Mkuu wa Shule ya Wasichana ya Mandera Ndugu Rose Ummy akimkabidhi risala Mlezi wa Shule hiyo Mama Salma Kikwete alipotembelea shuleni hapo tarehe 10.5.2014.
Mke wa Rais na Mlezi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mandera iliyoko wilayani Bagamoyo katika Mkoa wa Pwani Mama Salma Kikwete akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo mara baada ya kutembelea maeneo mbalimbali ya shule tarehe 10.5.2014.
Daktari Hadija Mwamtemi aliyefuatana na Mama Salma Kikwete anaonekana akimhudumia mwanafunzi (jina lake halikuweza kupatikana) wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Mandera aliyekuwa mgonjwa wakati Mama Salma alipotembelea shuleni hapo tarehe 10.5.2014.
Mke wa Rais na Mlezi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mandera Mama Salma Kikwete akiw\ katika picha ya pamoja na walimu na wafanyakazi wa shule hiyo na baadhi ya wageni waalikwa mara baada ya Mama Salma kuongea na wanafunzi na wafanyakazi wa shule hiyo tarehe 10.5.2014.
PICHA NA JOHN LUKUWI.