Watu 15 wameaga dunia katika msongamano uwanjani Kinshasa Ghasia.
Ghasia zilizozuka baada ya mechi ya soka timu mbili maarufu za Klabu ya ASV na Tout Puissant Mazembe zilipokuwa zikichuana katika mechi ambayo ingeamua muakilishi wa DRC katika kombe la bara Afrika mwakani.
Mwandishi wa BBC mjini Kinshasa anasema ghasia hizo zilianza dakika za mwisho za mechi baada ya timu ya Tout Puissant Mazembe kuongoza kwa bao moja na mashabiki wakaanza kurusha mawe uwanjani na kujeruhi baadhi ya wachezaji.
Refa alilazimika kusimamisha mechi hiyo.
Polisi walirusha gesi ya kutoa machozi ili kutawanya mashabiki waliokuwa wakipambana na kusababisha watu kuanza kukimbia na kukanyagana.
Gavana wa mji wa Kishasa amesema serikali itachunguza tukio hilo na waliohusika watachukuliwa hatua kali.
Chanzo: BBC