SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, April 22, 2014

Picha na Video:Umoja wa katiba ya wananchi-UKAWA- ambao unawaunganisha wabunge wa upinzani ndani ya bunge la katiba wamekutana Zanzibar na kutoa tamko la kuikataa hati ya muungano kuwa ni batili na hawana mpango wa kurudi bungeni hadi kieleweke.

 Mwenyekiti wa Chama cha CUF Mhe. Profesa Lipumba akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kutoka kwa Wajumbe wa UKAWA kutoka Vyama vya Upinzani Wanaohudhuria Bunge Maalum la Katiba
 Viongozi wa UKAWA wakiwa katika mkutano na Waandishi wa habari katika ukumbi wa hoteli ya Mzsons Shangani Zanzibar baada ya mkutano wao kuahirishwa na jeshi la Polisi Zanzibar kwa sababu za kiusalama .
 Mwenyekiti wa  CHADEMA, Mhe. Freeman Mbowe, akizungumza na waandishi wa habari sababu za kutoka katika bunge maalum la katiba Tanzania.akisisitiza jambo katika mkutano huo uliofanyika ukumbi wa hoteli ya Mazsons shangani Zanzibar.
 Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Mhe. James Mbatia akizungumza na waandishi katika ukumbi wa hoteli ya Mazsons Zanzibar.
 
 Baadhi wa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wa UKAWA waliotoka katika Kikao cha Bunge hilo wakiwa katika ukumbi wa hoteli ya Mazsons Shangani Zanzibar wakizungumza na waandishi wa habari.
 
  
Baadhi wa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wa UKAWA waliotoka katika Kikao cha Bunge hilo wakiwa katika ukumbi wa hoteli ya Mazsons Shangani Zanzibar wakizungumza na waandishi wa habari.