SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, April 2, 2014

MPINZANI WA MIYEYUSHO KUWASILI KESHO ASIBUHI





BONDIA Ronald Pontillas, atawasili nchini kesho asubuhi  kwa ajili yapambano lake la kimataifa dhidi ya bondia  Francis   Miyeyusho,litakalofanyika Jumamosi kwenye Ukumbi wa PTA, Dar es Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam jana, mratibu wa pambano hilo MussaKova, alisema kuwa Pontillas raia wa Ufilipino,  atawasili nchini
akiwa na kocha wake Amogo Samson.Kova alisema bondia huyo atawasili majira ya saa moja asubuhi,akitumia ndege ya Qatar Airways.

Alisema kuwa moja kwa moja ataenda hotelini kupomzika kablaya saa 5, kuzungumza na vyombo vya habari.Kova alisema kuwa maandalizi mengine yanaendelea vizuriambapo, hata suala la viingilio nalo tayari limeshapangwa.Alisema katika viingilio vitakuwa vya aina mbili ambavyo ni
sh.20,000 kwa VIP na kawaida itakuwa sh.10,000.
Alisema kuwa katika pambano hilo kutakuwa na mapambano ya
utangulizi ambayo atayatangaza kesho katika mkutano maalum na
vyombo vya habari.Pia  Kova alisema maandalizi yanakwenda vizuri na
kusisitiza kuwa litasimamiwa na chama cha  ngumi za kulipwa Tanzania (PST).
"Mabondia wote wako katika hali nzuri ya ushindani, tunategemea
Miyeyusho atafanya vizuri na kukabiliana na upinzani wa
mpinzani wake kwani ni bondia mzuri na mwenye kiwango cha
juu," alisema  Kova.