Airtel Tanzania imetangaza kuendelea kushirikiana na M-Heath Tanzania katika Kampeni ya Wazazi nipendeni baada ya kuwa na ushirikiano wa mwaka mmoja wenye mafanikio makubwa katika kuwasaidia kina mama wajawazito na watoto wachanga
Akiongea kuhusu mpango huo Meneja huduma kwa jamii Hawa Bayumi alisema” katika kutambua umuhimu na changamoto zinazoikumba sekta ya Afya ya uzazi, Airtel tumeonelea ni vyema tukashirikia na wenzetu wa M- Health katika kuwawezesha kina mama wajawazito kupata takarifa za afya ya uzazi kirahisi. Katika mwaka wa kwanza wa ushirikiano huu program hii imeweza kufanya vizuri kiasi cha kuchaguliwa kuwa huduma bora ya mobile heath katika kategori namba 1 ya Tuzo za Connected Life zinazotolewa na Global mobile Awards kila mwaka
Aliongeza kwa kusema wanawake nchini Tanzania wapo katika hatari ya vifo vya uzazi kwa uwiano wa 38:1 yaani kati ya wanawake 38 basi yuko 1 katika hiyo hatari na kila mwaka Tanzania inakumbwa na vifo vya watoto wachanga vyenye idadi ya kiasi cha watoto 48,100 ikiwa ni ya 10 kwa ukubwa duniani. Huduma ya ujumbe mfupi wa simu inawapatia watanzania , kina mama wajawazito na wamama wenye watoto wachanga hadi umri wa wiki 16 taarifa za afya kwa lugha ya Kiswahili bure yaani bila makato yoyote.
Airtel tunaahidi kuendelea kusaidia kampaini hii kwa kuendelea kuwawezesha wateja wetu waweze kupata huduma hii bure wakati wote na kuhakikisha tunachangia kikamilifu katika kutoa elimu na hatimae kusaidia kuboresha afya ya uzazi nchini.
Akiongea kwa niaba ya M- Health Tanzaania Mkurugenzi wa Mradi Janita Ferentinos alisema” tunapenda kuwashukuru sana Airtel kwa msaada wao mkubwa katika kuiwezesha kampaini hii kufanya vizuri. Ushirikiano wetu umetuwezesha kuwafikia watu wengi waliojiandikisha. Kwa watanzania wengi wanatumia huduma ya ujumbe mfupi zaidi , kwa kuondoa gharama na kufanya bure kumewezesha zaidi ya watanzania milioni 8 Tanzania kuweza kupata taarifa za msingi za afya ambazo zinaokoa maisha yao. Na ushirikiano huu umekuwa wa mafanikio kiasi cha mradi huu wa wazazi nipendeni kupewa Tuzo kama moja kati ya mpango bora wa M- Health duniani.