Eneo ambalo limeharibika kwa kuchimbika na kitu cha mripoko katika eneo
la mkunazini, na kuleta mtafaruku na tukio hilo la mripuko katika
majira ya mchana, Katika mripuko huo hakuna mtu aliyepata majarana na
uharibifu wa majengo katika eneo hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Mjini Unguja Mhe Abdi Mahmoud Mzee akizungumza na
Kiongozi wa Kanisa la Mkunazini Ndg. Nuhu Salanya, na Maofsa wa JWTZ ,
katika eneo la tukio na kutowa maelekezo kwa Uongozi wa Kanisa alipofika
katika eneo la tukio kuangalia athari na uharibifu uliotokea katika
eneo hilo, wakati wa mripuko huo.
Mkuu wa Wilaya ya Mjini Mhe Abdi Mahmoud Mzee akizungumza na Makamanda
wa JWTZ waliofika eneo la tukio kuagalia na kuchunguza tukio hilo la
mripoko katika eneo la Mkunazini jirani la Kanisani.
Maofisa wa JWTZ wakiangalia eneo la tukio lililochimbika kutokana na
kitu kinachodhaniwa ni bomu, katika tukio hilo hakuna Mwananchi
aliyejeruhiwa.




0 comments:
Post a Comment