SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, January 8, 2014

Zitto Kabwe apewa ushindi katika shauri lake la kipinga kujadiliwa.

Mahakama ya rufaa kanda ya Dar es Salaam imempa ushindi mbunge wa Kigoma kaskazini Mh. Zitto Kabwe katika shauri lake la kupinga kamati kuu ya chama chake kujadili uanachama wake hadi rufaa aliyokata baraza kuu la chama hicho itakaposikilizwa na kuamuliwa.
  Zitto akiwa ndani ya chemba namba moja ya Mahaka Kuu ambapo hukumu yake ya ushindi ilitolewa.
  Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia chama hicho, Zitto Zuberi Kabwe (katikati) akiingia Mahakama Kuu jana kusikiliza hukumu ya kesi yake ya kupinga Chadema kumjadili uanachama wake. Zitto Kabwe aliyekuwa akiwakilishwa na Wakili wake Albert Msando ambaye ji Diwani wa Chadema (kushoto kwa Zitto).
  Wakili wa Chadema katika kesi hiyo ambaye pia ni Mwanasheria wa chama hicho Tundu Lissu akizungumza na wana habari, kulia kwake ni wanachama wa chama hicho wakijifuta nyuso zao.
Tundu Lissu akiwatuliza wafuasi wa Chadema waliofurika mahakamani hapo jana kusikiliza kesi ya chama chao dhidi ya Zitto Kabwe.

0 comments:

Post a Comment