1
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Mh. Dk. Didas Masaburi (kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mashine maalum ya pili ya ‘TigoMatic’ inayopatikana Masaki jijini Dar es Salaam mapema. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja Tigo Bw. Zaem Khan
.
2
Meneja wa Huduma kwa Wateja Tigo Bw. Henry Mboya akimuonyesha Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Mh. Dk. Didas Masaburi jinsi mashine ya TigoMatic inavyoweza kufanya kazi katika kununua muda wa maongezi, kutuma na kupokea pesa, kulipia bili za huduma mbali mbali na kupata laini mpya ya simu.
3
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Mh. Dk. Didas Masaburi akionyesha kadi ya kipaumbele ya Tigo ambayo inatolewa kwa wateja waliokaa na Tigo kwa muda mrefu. Kadi hiyo inawezesha wateja kupatiwa huduma mbali mbali bila kupanga foleni na kuondokana na usumbufu wa gharama ndogo ndogo pindi watakapofika katika matawi yeyote ya Tigo kuhudumiwa. 
4a
stahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Mh. Dk. Didas Masaburi akitoa hotuba yake. Mstahiki Meya huyo aliipongeza Tigo kufanikiwa kuwa kampuni ya simu ya kwanza nchini Tanzania kuanzisha huduma hiyo za mashine maalum za TigoMatic.
5a
Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja Tigo Bw. Zaem Khan akimshukuru Mstahiki Meya, waandishi wa habari na wegeni wengine waalikwa kwa kufika katika uzinduzi huo. Mashine ya TigoMatic itakuwa wazi kwa masaa ishirini na nne kila siku.
Tigo Tanzania  imezindua mashine maalum ya pili ya TigoMatic inayowawezesha wateja wake kulipia bili za huduma mbali mbali na kuongeza salio itakayofanya kazi kwa masaa ishirini na nne kwa siku.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na Meya wa jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Masaburi, ambaye ameipongeza Tigo kwa kuwa kampuni ya mawasiliano kwanza nchini Tanzania kuanzisha huduma ya aina hiyo nchini.
“Ubunifu huu wa Tigo si tu wa manufaa kwa wateja wake bali pia ni hatua mojawapo kubwa ya kimaendeleo kwa nchi yetu katika matumizi ya teknolojia za mawasiliano za kisasa duniani katika sekta ya mawasiliano,” alisema Dk Masaburi. 
Dk Masaburi alisema huduma mbalimbali zitolewazo na makampuni ya simu zikiwemo kupiga simu, SMS, intaneti pamoja na huduma za kutuma na kupokea fedha zimeleta mageuzi chnaya katika ufanyaji biashara na kuchangia kuboresha maisha ya mamilioni ya watanzania.
Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika katika tawi la huduma kwa wateja la Tigo lililopo Masaki, Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja Tigo Bw. Zaeem Khan, amesema uzinduzi wa ‘TigoMatic’ utawawezesha wateja wa Masaki kupata huduma za zitolewazo na Tigo kwa masaa ishirini na nne kwa siku.
“Habari njema kwa watu wa Masaki ni kwamba hakutakuwa na ulazima tena kwa wateja kukaa kwenye foleni kwa ajili ya kupata huduma kutoka kwenye matawi yetu na sehemu nyinginezo za mauzo kwa sababu mashine hii ya TigoMatic inatoa msaada wa mteja kujihudumia mwenyewe,” alisema Bw. Khan.
Hii ni mashine ya TigoMatic ya pili kuzinduliwa jijini Dar es Salaam na kampuni ya simu Tigo. Mwezi uliopita Tigo ilikuwa kampuni ya simu ya kwanza nchini kuzindua matumizi ya aina hii ya mashine ilipoanza kutoa huduma hii katika tawi la makao makuu ya kampuni hiyo yaliyoko Kijitonyama.
Akielezea jinsi mashine hizo zinavyofanya kazi, Bw. Khan alisema TigoMatic ni mashine ambazo mteja anaweza akajihudumia yeye mwenyewe kama ilivyo kwa mashine za kibenki za ATM ambapo mteja anaweza akafanya miamala tofauti tofauti bila kuhitaji kuhudumiwa na mfanyakazi wa benki. Alisema kwamba wateja wa Tigo hawatakuwa na ulazima wa kujisajili upya kwa ajili ya kutumia mashine hizo. 
Khan alisema kampuni inaazimia kuweka mashine zake katika matawi yake yote ya huduma kwa wateja nchi nzima pamoja na sehemu za mikusanyiko mikubwa ya watu kama vile maduka makubwa, stendi za mabasi, mitaani, viwanja vya michezo na mahospitalini.