SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, January 16, 2014

Rais Jakaya Kikwete Awaapisha Balozi Mpya wa Tanzania Nchini Malaysia na Kamishna wa Tume ya usuluhishi na Uamuzi

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wateule aliowaapisha ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Kushoto ni Kamishna wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi Bwana Jafari Omari na kulia ni Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia Dkt.Aziz Ponary Mlima.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo asubuhi amewaapisha Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia na Kamishna wa Tume ya usuluhishi na Uamuzi.Walioapishwa leo katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam ni Dkt. Aziz Ponary Mlima anayekuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia na Bwana Jafari Omari  anayekuwa Kamishna wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi. Pichani ni Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Aziz Ponary Mlima akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo.
 Kamishna wa Tume ya usuluhishi na uamuzi Bwana Jafari Omari akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Picha na Freddy Maro-IKULU

0 comments:

Post a Comment