Mh
Juma Ngasongwa akikokotwa kuingizwa Hospitali ya Tumbi kupatiwa matibabu
baada ya kupata ajali katika eneo la Kibaha jana jioni. Mhe. Ngasoma
amenusurika kifo katika ajali hiyo iliyotokea jana jioni Kibaha Picha ya
ndege Mkoani Pwani
Mkuu
wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza na Dr Loti Kiwelu akimjulia hali
katika Hospitali ya Tumbi Kibaha alipofikishwa kwa ajili ya huduma ya
kwanza ambapo alihamishiwa katika Hosipitali ya Muhimbili MOI kwa ajili
ya matibabu zaidi.
Ajali
hiyo ilihusisha gari aina ya Rav 4 mali ya Ngasongwa ambaye alikuwa
akiendesha mwenyewe kutoka jijini Dar es salaam kuelekea Morogoro ambapo
kwa mujibu wa Ngasongwa alichomekewa na lori la Tanesco pichani chini.
Gari la Ngasongwa likiwa limeharibika vibaya.
Lori la Tanesco lililosababisha ajali hiyo.Picha na Chris Mfinanga
0 comments:
Post a Comment