SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, January 13, 2014

MBUNGE WA TEMEKE-CCM ABBAS MTEMVU KUKISAMBARATISHA KIKUNDI CHA VIJANA TISHIO CHA MBWA MWITU TEMEKE


 Mbunge wa Jimbo la Temeke Dar es Salaam, Abbas Mtemvu akihutubia katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya Kata ya YOmbo Kilakala, leo, ambapo aliwaambia kuwa hatolifumbia mamcho  kulitokomeza kundi la  vijana la Mbwa Mwitu linalotishia usalama wa wananchi katika kata hiyo.Kutoka kulia mstari wa mbele ni Diwani wa Viti Maalumu, Wilaya ya Temeke, Mariam Mtemvu. Katibu wa Siasa na Uenezi Wilaya ya Temeke, Rutami  Mabunu,  Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kilakala  na Shomari Lyoto ambaye ni Katibu wa Kata hiyo. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Kada wa CCM, Mwishehe Kilakala akijitambulisha katika mkutano huo.
 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Kata ya Yombo Kilakala wakiwa katika mkutano huo
 Ofisa Mtendaji wa Kata ya Yombo Kilakala, Peter Makoye akitoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho. Kiasi kikubwa cha taarifa hiyo ilikataliwa na wajumbe kwamba haikuwa ya kweli.
 Camillius Haule  ambaye ni Katibu wa Uenezi wa Mtaa wa Kiembe Samaki, akielezea jinsi vijana wahalifu wanaoojiita Mbwa Mwiti wanavyotishia usalama wa wananchi katika kata hiyo.
 Mjumbe wa Kamati ya Mipango Kata ya Yombo Kilakala, Nasir Kinyogoli, akielezea ubadhilifu wa fedha za Ukimwi na Vicoba katika Kata hiyo.
 Asmah Zitiakielezea tatizo la walimu katika Shule ya Msingi Kigunga kuwachapa viboko wanafunzi kwa kukosa fedha za kulipia Tuisheni.
Katibu wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Kata ya Yombo Kilakala,FatumaMgendo akielezea masikitiko  kuhusu kitendo cha walimu wa Shule ya Msingi kwachapa viboko wanafunzi kwa kukosa hela ya kulipia tuisheni.

0 comments:

Post a Comment