SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, January 13, 2014

KAMPUNI YA VIJANA WA KITANZANIA YA (CHINA WORD BUZ) KUWAKOMBOA WAFANYABIASHARA WADOGO NA WA KATI‏,

2
Meneja Mkuu wa kampuni hiyo nchini China Justin Luvanda akizungumza na waandishi wa habari kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara baada ya kwasili akitokea nchini China na ujumbe wa wafanya biashara wenzake, kushoto ni Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya China Word Buz nchini China Bwana Cheng Wang Wu na kulia ni Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo hapa nchini Bw. Shafii Mwaijande.
1
Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya China Word Buz na mwakilishi wa wamiliki wa viwanda 45 nchini China vilivyoingia mkataba wa kibiashara na kampuni hiyo China Bwana Cheng Wang Wu kushoto akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere huku akiwa ameongozana na Meneja Mkuu wa kampuni hiyo nchini China Justin Luvanda wakilakiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo hapa nchini Bw. Shafii Mwaijande, kampuni hiyo imeanzishwa nchini ikiwa na lengo la kuwakomboa na kuwasaidia wafanya biashara wadogo na wa kati nchini Tanzania ili kutafuta masoko na kuwapa taarifa sahihi za masoko na biashara nchini China ambapo wanatarajia kuendesha semina kwa wafanya biashara katika mikoa ya Dar es salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya.
 3
Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo hapa nchini Bw. Shafii Mwaijande wa pili kutoka kulia, Meneja Mkuu wa kampuni hiyo nchini China Justin Luvanda wa tatu kutoka kulia na Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya China Word Buz nchini China Bwana Cheng Wang Wu wa tatu kutoka kushoto wakiwa na wafanya biashara wenzao.
4
Meneja Mkuu wa kampuni hiyo nchini China Justin Luvanda akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari.

0 comments:

Post a Comment