SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, January 18, 2014

KIKAO CHA KUKAMILISHA "UKAGUZI MAALUM "EXIT MEETING" CHA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI,CHAMFUTA KAZI MEYA WA BUKOBA JANA

Katibu tawala Mkoa, Mkuu wa mkoa Kagera Mh. Fabian Massawe, Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kutoka Jamh
uri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Ludovick Utouh wakiingia ukumbini leo Bukoba.
Mkuu wa mkoa Kagera Mh. Fabian Massawe, Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Ludovick Utouh
Katibu Tawala wa Mkoa Kagera Bw. Nassor Mnambila akisoma taarifa yake wakati wa Mkutano huo.
Mkuu wa mkoa wa Kagera Mh.Fabian Massawe akimkaribisha mgeni Rasmi leo kwenye kikao hicho cha kukamilisha Ukaguzi Maalum" Exit Meeting"  Cha mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali leo Januari 17.2014 Mjini Bukoba ambapo kikao hicho kilianza mapema saa 5 Asubuhi.
Taswira Ukumbini
Meya wa Manispaa ya Bukoba, Anatory Amani (kulia) pamoja na Madiwani wa Manispaa ya Bukoba ambapo swala kubwa kwa Madiwani....wanamtuhumu ndugu yao Meya kwa matumizi mabaya ya madaraka.Mkurugenzi mpya wa manispaa ya bukoba Ambekiswe shemwela
 Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Ludovick Utouh (kulia) ambaye alikuwa ni mwakilishi wa Waziri Mkuu, akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Bw. Fabian Massawe katika Meza kuu.
Bw. Ludovick Utouh ameambatana na Bw. Mero, Bi Mwadawa A. Mgendera na Bw. Elisha M. Nkwija pamoja na Bw. Sabuni ambao wameshiriki kufanya ukaguzi Bukoba Mjini.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Ludovick Utouh akitoa taarifa ya ukaguzi maalum leo Bukoba.
Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri  (katikati) ambaye pia alimwakilisha Waziri mkuu akimsikiliza kwa makini Bw. Ludovick Utouh
Viongozi wakifuatilia kwa makini
Viongozi Meza kuu wote walikuwa makini  kusikiliza taarifa hiyo Muhimu ya Ukaguzi.
Bw. Ludovick Utouh akiendelea kutoa Taarifa ya Ukaguzi maalum leo
Taswira ya kikao chenyewe ndani
Waheshimiwa Madiwani wa Manispaa ya Bukoba kulia ni Mstahiki Meya Anathory Amani ambaye madiwani wa manispaa wanamtuhumu kwa matumizi mabaya ya madaraka.
CAG akiendelea na kazi!
Furaha hapa!!
Mkurugezi wa Manispaa Bukoba( kulia) Bw.Limbakisye Shimwela
Mkurugezi wa Manispaa Bukoba (kulia) Bw. Limbakisye Shimwela akiwa na viongozi wengine wakisikiliza taarifa ya ukaguzi leo
Taswira Ukumbini leo wakati wa kikao cha kukamilisha Ukaguzi maalum Mkoani hapa Kagera
Mstahiki Meya Anatory Amani (kulia) kushoto ni Mzee Rwangisa, Ukumbuke pia Mzee huyo Rwangisa ndiye aliyemwachia nafasi Meya Anatory Amani.
Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri ndie aliyemalizia kwa kutoa Maelezo ya Serikali.
Baadhi ya Madiwani wakisikiliza kwa makini.
Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri akiendelea kutoa Maelezo ya Serikali. Kuhusu Suruhisho hilo ambapo yamebainika Makosa ya Meya Anatory kufanya makubaliano bila idhini ya Madiwani na Taratibu za serikali, Basi ajipime Mwenyewe na Kujiudhuru mara moja kwa Maslahi ya Manispaa ya Bukoba.
Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri akiendelea kutoa maelezo ya serikali kiujumla na kukamilisha ukaguzi huo. 
Watumishi wa Manispaa wachukuliwe hatua 
Bw. Khamis Kaputa avuliwe Madaraka 
Mhandisi,Mweka hazina nk wapoteze vyeo vyao! 
Wakandarasi wote waliopata fedha bila taratibu wazirejeshe.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh.Fabian Massawe (kulia) akisikitika baada ya kumsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri ambaye aliyemwakilisha vyema Waziri Mkuu.
Katibu Tawala wa Mkoa Kagera Bw. Nassor Mnambila kushoto nae akisikitika leo kwenye "Exit Meeting"
 
**Muda mfupi baadae uliopita Meya ametangaza kujiuzulu nafasi yake baada ya ripoti ya CAG kusomwa na kubaini mapungufu makubwa**

0 comments:

Post a Comment