Msafara
wa Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana ukipita leo katika
'mkeka' wa barabara, ulipokuwa ukitokea wilayani Namtumbo kwenda
wilayani Songea mkoani Ruvuma.Ndugu Kinana yuko katika ziara mkoani
Ruvuma, kukagua utelekezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM, kusikiliza kero
za wananchi na kushirikiana nao kupata njia za kuzitatua, barabara hiyo
ni miongoni mwa barabara kadhaa zilizojengwa katika maeneo mbalimbali
nchini ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya CCM na kuwaondolea wananchi kero
ya kusafiri kwenye barabara mbovu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki shughuli za ujenzi katika Zahanati ya Mahilo wilayani Songea mjini .
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba ya mwalimu
kwenye shule ya sekondari Mdandamo wilayani Songea mjini
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikagua ujenzi wa nyumba ya maabara katika shule ya sekondari Mdandamo wilayani Songea mjini
Katibu
wa NEC, Itikati na Uenezi Nape Nnauye akishirikiana na Mwenyekiti wa
CCM mkoa wai Ruvuma, kuondosha gogo kwenye eneo la ujenzi wa Zahanati
katika Kata ya Mahilo, Songea mkoani Ruvuma.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na
waasisi wa CCM wilaya ya Songea mjini, kutoka kushoto ni Mzee Hashimu
Gawaza na kulia kwa Katibu Mkuu ni Mzee Clemenci Nyoni ambao walikaa
kikao cha kwanza na Mwalimu Nyerere tarehe 12 Agosti 1957 wakati wa
harakati za kuikomboa nchi,anayefuatia kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa
wa Ruvuma Ndugu Oddo Mwisho.
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akiwa na Wazee hao.
Katibu
Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wazee waasisi pamoja na
wananchi wa kata ya Matogoro ambapo alitaka wana CCM kuenzi kazi
zilizofanywa na waasisi wetu kwa kudumisha mshikamano ,umoja na amani.
Ofisi
ya Kata ya Matogoro CCM ambayo iliwekwa jiwe la msingi tarehe 20
Desemba 1986 na Mzee Rashid Mfaume Kawawa,Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana ameahidi kutoa bati za kuezeka ofisi hiyo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchama wa Shina
namba 1tawi la Ambachai kata ya Mfaranyaki nyumbani kwa Balozi wa Shina
Ndugu Magreth Mchula,Katibu Mkuu alisisitiza viongozi wa ngazi za chama
kuwa na mazoea ya kutembelea mabalozi wao kwani ndio msingi wa
wanachama.
Wanachama
wa Shina namba 1 wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana,pichani Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa
amejumuika na wanachama kukaa nao pamoja kwenye mkeka.
Mzee
Mustafa Mohamed Songambele akionyesha furaha yake alipokutana na Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana , Mfaranyaki Songea,Katibu Mkuu
ameanza leo ziara ya kuetembelea wilaya ya Songea mjini.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na viongozi
mbalimbali wa CCM waliofika kumlaki alipowasili kwenye eneo maarufu
linalojulikana kama Nonga Nonga wilaya ya Songea mjini.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akisalimiana na Mzee Mustafa Songambele mmoja wa waasisi wa Tanu na mwanasiasa wa muda mrefu.
Mlezi
wa Vijana wajasiriamali wa Mfaranyaki Dk.Asha-Rose Migiro akiwasalimu
vijana hao baada ya kufunguliwa kwa Shina lao na Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia ngoma ya kutoka kikundi
cha ngoma cha Mfaranyaki baada ya kuzindua shina la vijana
wajasiriamali wa Mfaranyaki.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishirikiana na wananchi wa Kata hiyo
kusafisha eneo kwenye ujenzi wa Zahanati ya kata hiyo. Wanne kulia ni
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
Wazee
pekee wawili walisosalia kati ya waliokuwepo kwenye mkutano wa Baba wa
Taifa Mwalimu Nyerere wakati wa harakati za TANU, mwaka 1957 katika eneo
la Matogolo, Songea mkoani Ruvuma, Hashim Gawaza (92) na Clemence Simon
Nyoni (93), wakivishwa vazi la heshima na Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana, alipowasili eneo hilo leo
Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kushoto) akiwa na wanachama wa
Shina namba noja, waliokuwa wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana, alipotembelea nyumbani kwa Mjumbe wa Shina namba
moja, Magreth Mtiula, eneo la Mfaranyaki mjini Songea.
Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimsalimia mama huyu, Mkazi wa
mtaa wa Mfaranyaki mjini Songea, baada ya kumuona kuwa mwenye shangwe
kubwa wakati msafara wa Kinana ulipopita karibu na nyumbani kwa mkazi
huyo.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akifungua Shina la Vijana Wajasiriamali
wa CCM la Dk. Asha-Rose Migiro, katika mtaa wa Mfaranyaki mjini Songea
leo
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akisalimia baada ya kuzinduliwa shina hilo.
0 comments:
Post a Comment