Ndugu zangu,
Leo asubuhi karibu nikione cha mtema kuni. Nilipokuwa kwenye jogging nikapandisha nikikimbia mpaka juu ya Mlima Gangilonga.
Huko nikaiona picha nzuri ya kuipiga. Mzee Mtema Kuni na mbwa wake sita.
Nikamsalimia Mzee yule kwa Kihehe. Kisha nikamwomba nipige picha. Akanijibu kwa Kihehe kuwa ni sawa.
Basi, Mzee naye akaanza kujiendea zake
porini huku mbwa zake sita wakiwa wamelala chini. Kumbe, mbwa
hawakufurahia, maana, nilipoanza tu kupiga picha ya kwanza, wakainuka
wakibwaka na kunijia kutaka kunishambulia. Na kwa mbwa wale, kauli ile
ya mwenye mbwa ya kuwataka kutulia hawakuisikiliza kabisa.
Nami nikiwa peke yangu sikuwa hata na
jiwe la kuokota kuwatishia mbwa wale. Lakini, inasemwa, ukimya na
utulivu ni silaha pia. Nilisimama wima nikiwa nimetulia tuli.
Na utulivu wangu ule ulionekana
kuwashangaza mbwa wale. Bila shaka walishangazwa sana na kujiamini
kwangu kule. Hawakujua kuwa sikuwa na cha kufanya, na kuwa kama
wangetaka kunivamia wala wasingepata tabu kunitia adabu.
Naam, wakati mwingine haisaidii kuongea na mwenye mbwa! Busara ni kuongea na mbwa wenyewe kwanza!
Maggid Mjengwa.
Iringa.
Maggid Mjengwa.
Iringa.
0 comments:
Post a Comment