Meza kuu ya viongozi wa
matawi ya CCM New York na DC wakimsikiliza msimamizi na msemaji mkuu wa mkutano
huo bwana Isaac Kibodya. Mkutano wa CCM tawi la New York ulifanyika kwa
mafanikio makubwa. Na hii ni mara ya kwanza kwa New York kuwa na tawi na kuweza
kufanyika mkutano kama huu. Dhumuni la mkutano huo ni kuhamasisha Watanzania
kujiunga na chama na kuchukua kadi hili mchakato wa kuchagua viongozi wapya
watakao tambulika kichama na kiserikali.
Msimamizi wa mkutano huo
Bwana Isaac Kibodya akizungumza, maneno muhimu ambayo bwana Kibodya alisisitiza
katika mkutano huo ni kwanza ni mshikamano na umoja wa watanzania, pili ndiyo
chama. Kwa sababu bila mshikamano kama watanzania hakuwezi kuwa na chama
imara.
Katibu wamuda wa tawi Bwana
Mseba akizungumza mbele ya wanachama katika mkutano huo. Bwana Mseba ndiyo
mwimili mkubwa wa tawi la CCM New York.
Professor Lwiza Kamazima
kati ya watu walikuwa bega kwa bega na Bwana Isaac Kibodya kufanikisha mkutano
huo wa CCM kufanyika. Moyo wa kujitolea wa Profesa Lwiza ndiyo mafanikio ya
kuwepo kwa mkutano huu kwa mara ya kwanza ndani ya jiji la wasiyo lala
NYC.
Loveness Mamuya au (Iron
Lady) akiongea katika mkutano huo. Loveness kutoka DC ndiyo chanzo na chimbuko
cha matawi yote ya CCM Marekani. Licha ya zengwe na kalinjekalinje alizokumbana
nazo kwenye harakati za kufanisha kuwepo kwa matawi ya CCM Marekani lakini
hakutetereka na kurudisha moyo wake nyuma. Loveness kasimama kidete kama
mwanamke jasiri na kuyashinda majaribu yote.
Mwenyeketi wa muda wa tawi
la CCM New York Bwana Mafutah akiongea jambo kwenye mkutano huo. Bwana Mafutah
alikuwa Tanzania na alipata fursa ya kukutana na viongozi mbalimbali wa
CCM.
Mzee Sebo mwenyekiti wa
tawi la CCM DC akiongea machache katika mkutano huo. Kushoto kwake na Iron Lady
Loveness na kulia kwa Mzee Sebo na Mafutah.
Mwanamusic wa kizazi kipya
anaetamba na ngoma yake mpya inayojulikana kwa cheza cheza bila kukunja goti
MwanaFA alikuwepo pia kutoa hamasa katika mkutano huo.
Watanzania waliojitokeza
kwenye mkutano huo wakisikiliza kilichokuwa kinaendelea.
Mwenyekiti wa New York
Tanzania Community Bwana Hajji Khamis alikuwepo pia kusikiliza kinachojili
mkutanoni hapo
Wanachama wa CCM kutoka
Springfield waliwepo pia kwenye mkutano huo
Mkuu wa wilaya ya
Springfield Bwana Isaac Kibodya akipata ukodac na Dullar wa
Brooklyn.
Mweka hazina wa CCM tawi la
DC kushoto akipiga ukodac na Bwana Mseba kulia
Dr Temba akipata ukodak na
wageni kutoka DC.
Team kutoka DC ikipata
ukodak.
Dr Temba akipata ukodak na
mgeni kutoka DC.
Viongozi wa tawi la CCM DC
wakipata ukodak wakiwa kwenye meza kuu.
Dr Temba na rafikia yake
Stanley
Mbuyu nao ulianza kama
mchicha CCM Oyee
NA MICHUZI MATUKIO
0 comments:
Post a Comment