Waziri wa Nchi , Ofisi ya
Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu (kulia) akimkabidhi nyaraka
za utendaji kazi mwenyekiti wa Baraza jipya la Taifa la Uwezeshaji
Wananchi Kiuchumi Bw. Omari Issa wakati wa uzinduzi wa baraza hilo leo
jijini Dar es salaam
Mwenyekiti
wa Baraza jipya la Taifa
la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bw. Omari Issa akizungumza na wajumbe wa baraza
hilo mara baada ya uzinduzi leo jijini Dar es salaam
Waziri
wa Nchi , Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu
akizungumza na wajumbe wa Baraza jipya la Taifa la Uwezeshaji
Wananchi Kiuchumi wakati wa uzinduzi wa baraza hilo leo jijini Dar es
salaam
Waziri
wa Nchi , Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu (katikati) akizungumza jambo na
Mwenyekiti wa Baraza jipya la Taifa la Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi Bw. Omari Issa (kushoto) na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt.
Anacleti Kashuliza leo jijini Dar es salaam
Wajumbe
na Viongozi wa Baraza jipya la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Wakiwa katika picha
ya pamoja na Waziri wa
Nchi , Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu.
----
Na.
Aron Msigwa
Serikali
imesema kuwa itaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wananchi
waliojiunga katika vikundi vya ujasiriamali katika maeneo mbalimbali nchini.
Kauli
hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Nchi , Ofisi ya
Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu wakati akizindua
Baraza jipya la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi .
Amesema
kuwa serikali inatambua na inaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na
wananchi katika kujiletea maendeleo kupitia ushiriki walio nao katika vikundi
mbalimbali walivyovianzisha katika maeneo yao na kufafanua kuwa serikali
kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu inaendelea kuunga mkono juhudi hizo kwa
kuanzisha Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.
Dkt.
Nagu amesema kuwa Baraza hilo lina jukumu kubwa la kusimamia na kuratibu
utekelezaji wa sera ya Taifa ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi ya mwaka 2004 na
kufafanua kuwa utekelezaji wa mikakati na malengo ya Dira ya maendeleo
ya mwaka 2025 ya kuiwezesha Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati itaweza
kufikiwa iwapo watanzania watashiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo.
Ameongeza
kuwa Baraza hilo lina jukumu la kuwaelimisha wananchi kuhusu tafsiri ya
uwezeshaji Wananchi kiuchumi ambayo kwa muda mrefu imekua ikipotoshwa na
kusisitiza kuwa dhana ya uwezeshaji sio kupitia mitaji pekee bali ni kujenga
uwezo wa wananchi kuweza kuziona fursa zinazowazunguka na kuweza kuzitumia kwa
maendeleo yao.
“
Nchi zinazoweza kuendelea ni zile ambazo zimejenga uwezo kwenye ushirika,
lazima tuvijenge uwezo vikundi vyetu vya maendeleo ili tuweze kugundua wapi
tunakwama na namna ya kutatua changamoto zilizopo ili tupige hatua, kwa sababu
maana ya uwezeshaji sio tu kupata mitaji au kupewa mikopo, wapo watu tayari
wana mitaji lakini hawawezi kufanya lolote hao tunachokifanya tunawajengea
uwezo” Amesisitiza Dkt. Nagu.
Ameeleza
kuwa ipo haja kwa vikundi mbalimbali vilivyojiunga katika ushirika kuendelea
kujenga uwezo ili viweze kufanya makubwa na kuaminiwa na wadau mbalimbali
pamoja na serikali huku akitoa mfano wa uamuzi wa serikali kununua samani
zinazotengenezwa na watanzania.
Dkt.
Nagu amesema kuwa serikali imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali ya uboreshaji
wa miundombinu inayolenga kuwawezesha wananchi kiuchumi ikiwemo huduma za afya
na elimu na kuwataka wajumbe wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kuweka
umuhimu katika maeneo yatakayoleta matokeo ya haraka na yanayogusa maisha ya
wananchi wengi hususan kwenye kilimo, Ufugaji, Uvuvi, Misitu,Ufugaji Nyuki na
Utalii.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Baraza hilo Bw. Omari Issa akizungumza mara baada ya
kuzinduliwa kwa baraza hilo amesema baraza hilo litaendelea kuwajengea uwezo
wananchi kuzitumia fursa zinazowazunguka kujiletea maendeleo.
Amesema
baraza litaendelea kutoa elimu kwa wananchi kwa kuwahamasisha kujenga uwezo katika
vikundi vya ushirika ili waweze kumiliki uchumi wa nchi huku akifafanua kuwa
wananchi walio wengi wanahitaji elimu kuhusu dhana ya uwezeshaji Kiuchumi na
namna ya kutumia fursa na mikopo wanayopata kutoka katika taasisi mbalimbali za
fedha kupata faida .
Baraza
hilo lenye wajumbe 9 litadumu kwa miaka 3 huku likiwa na jukumu la kuhakikisha
linawasaidia wananchi kumiliki na kunufaika na fursa za kiuchumi zilizopo
nchini.
0 comments:
Post a Comment