SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, October 26, 2013

Msiba wa Martha Shani DC na mapambano dhidi ya uvutaji sigara nchini Marekani

Marehemu Martha Shani

 Hivi punde tutasikia taarifa ya harakati za kuzuia uvutaji sigara nchini Marekani ambazo sasa zimeamsha wasiwasi mwingine baada ya kugundulika kuwa harakati hizohizo zimeifanya idadi ya wavutaji walio kati ya darasa la 6-12 kuongezeka maradufu.Lakini kwanza tuangalie habari za msiba ulioikumba jamii ya waTanzania waishio maeneo ya Washington DC.

Uvutaji sigara, ni sababu kubwa ya vifo vinavyozuilika nchini Marekani. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Kituo cha Kudhibiti Maradhi nchini Marekani (CDC) kifo kimoja kati ya vitano nchini Marekani hutokana na athari za uvutaji sigara, na zaidi ya watu milioni 43.8 nchini humo ni wavutaji wa sigara.

Lakini vita dhidi ya uvutaji huo vimekuwa vikipamba moto, na teknolojia imekuwa ikishirikishwa katika vita hivyo. Na ni vita hivyohivyo dhidi ya uvutaji vinavyoanza kutiliwa mashaka nchini humo.

Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).


Hii ilikuwa ripoti ya Oktoba 26, 2013
 

0 comments:

Post a Comment