SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, October 26, 2013

JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA NA VODACOM WAWAKUMBUKA YATIMA IRINGA

Mwakilishi  wa Vodacom mikoa ya nyanda  za  juu  kusini kati na mjumbe  wa  bodi ya wakurugenzi  wa  jukwaa la wahariri nchini Tanzania Masoud Sanani (kushoto)  wakikabidhi msaada  wa chakula na  vitu  mbali mbali  kwa  mkuu wa  kituo cha yatima  cha Huruma  Center mjini Iringa  Bi Costansia Chilewa ,msaada uliotolewa  jukwaaa la  wahariri kwa  ufadhili  wa Voda Com Tanzania
 Mwakilishi  wa Vodacom akimkabidhi  msaada  mkuu wa  kituo cha yatima  cha Huruma  Center huku mwakilishi wa jukwaa la  wahariri Bw Masoud Sanani akishuhudia
 Baadhi ya  wahariri  nchini Tanzania na wafanyakazi  wa Vodacom wakiwa katika  picha ya pamoja na baadhi ya  watoto yatima  wa  kituo cha Huruma Center  Iringa baada ya  kuwakabidhi  misaada mbali mbali iliyotolewa na jukwaa la  wahariri kwa ufadhili wa Voda  Com Tanzania
 Baadhi ya  wahariri na  wafanyakazi  wa Voda  com Tanzania  wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kushusha msaada  wa chakula  uliotolewa na  jukwaaa hilo na  Vodacom Tanzania
 Mwakilishi  wa  jukwaa la  wahariri Bw  Masoud Sanani akipongezwa na mkuu wa  kituo  cha Huruma  Center Bi Costansia Chilewa kwa msaada  huo
 Baadhi ya  watoto  yatima  wa kituo cha Huruma  Center Iringa  waliopatiwa msaada na jukwaa la  wahariri  na Vodacom Tanzania
 Magari  ya Vodacom yaliyopeleka msaada  kituoni hapo
Wahariri  wa  vyombo vya habari na wanahabari pamoja na  wafanyakazi wa Vodacom wakiondoka  kituoni hapo baada ya  kukabidhi msaada  wao 

****
Na  Francis Godwin Blog
JUKWAA la  wahariri nchini  Tanzania  kwa  kushirikiana na kampuni ya  simu ya Vodacom Tanzania  wamekabidhi msaada  wa  chakula  na  vitu mbali mbali kwa kituo cha yatima  cha Huruma  Center mjini Iringa.
Akikabidhi  msaada  huo jana  kwa niaba ya  jukwaa la  wahariri Tanzania mjumbe wa  bodi ya wakurugenzi  ya kuwaaa la  wahariri nchini Bw Masoud Sanani  alisema  kuwa  jukwaa la  wahariri  limetoa msaada  huo kwa ufadhili wa kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom Tanzania .
Alisema  kuwa  imekuwa ni kawaida ya  jukwaa  hilo la  wahariri kwa kushirikiana na  wadau mbali mbali kila mwaka   kutembelea na kusaidia watoto  yatima wa eneo  ambalo jukwaa  hilo litafanya mkutano  wake mkuu.
Hivyo  alisema  kutokana na mwaka  huu mkoa  wa Iringa  kuteuliwa kuwa  mwenyeji  wa mkutano huo  wa jukwaa la  wahariri ,mkutano  utakaomalizika  leo wamelazimika kutembelea  kituo hicho na  kuungana na  watanzania  wengine katika  kuwasaidia   watoto  hao.
Bw Sanani mbali ya  kupongeza  jitihada za Voda  Com Tanzania  kwa kujitolea  kudhamini  zoezi hilo bado  alisema kuwa  kinachofanywa na wahariri  pamoja na  wadhamini hao ni sehemu  ya  kuonyesha kuwa  jukumu la kuwasaidia  yatima  ni la kila mtanzania kwa nafasi aliyonayo na  si vema jamii  kuendelea  kuwatenga  watoto  hao.
Hata  hivyo  aliwataka  watoto hao  yatima  kuongeza jitihada katika masomo na  kuacha  kusononeka  na hali  hiyo ya uyatima   walionayo kwani jamii  bado  itaendelea  kuwakumbuka  zaidi.
Kwa  upande wake mkuu  wa kituo hicho Bi Costansia Chelewa akishukuru Voda Com na Jukwaa la  wahariri kwa msaada  huo alisema  kuwa msaada  huo ni  miongoni mwa misaada mikubwa  kutolewa  kituoni hapo  na kuwa wao kama  kituo  wanawapongeza wahariri na Voda com  kwa jitihada  hizo.

Alisema  kuwa  kituo hicho  kinamilikiwa na kanisa la kiinjili la  kirutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa na kina  watoto zaidi ya 50  huku moja kati ya mikakati ya  kituo ni kuja kuanzisha  miradi ya  kujitegemea  ili  kuwafanya  watoto hao  kuwa na miradi yao.
Kuhusu  changamoto kubwa inayowakabili  watoto  hao alisema ni pamoja na  walimu kurudisha  kituoni  mara kwa mara  kutokana na michango mbali mbali ambayo  wamekuwa  wakitakiwa  kulipa shule za msingi
NA MICHUZI MATUKIO BLOG

0 comments:

Post a Comment