SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, October 23, 2013

Majina ya vyuo 9 vilivyofutwa na Serikali kwa kukosa sifa

mulugo_816c8.jpg
Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imevifuta vyuo ambavyo havina sifa ikiwamo kukosa usajili wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) na kufundishwa na walimu wasio na sifa. Vyuo vilivyotangazwa kufutwa ni:
-
1. Media and Values Training Institute (Dar es Salaam)
2. Information Technology Training Center (Dar es Salaam)
3. Dar es Salaam School of Hair Design (Dar es Salaam)
4. Morogoro School of Medical Sciences (Morogoro)
5. Media and Research Center
6. Vision Hotel and Tourism College
7. East Africa College of Hospitality and Tourism
8. The Africa Institute of Business Management
9. Aspiration Training Center 
Naibu Waziri wa Wizara husika , Philip Mulugo, alitangaza hatua hiyo wakati alipokutana na Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Profesa Sifuni Mchome, alisema Serikali ilishatangaza kuwa vyuo visivyo na sifa vifungwe lakini tatizo likawa ni jinsi ya kuwatafutia wanafunzi waliopo vyuo vingine.
Source: http://www.wavuti.com

0 comments:

Post a Comment