SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, October 20, 2013

Kuondoka Kwa Anko J...

995199_10201507856431059_503138343_n_0967e.jpg
Ndugu zangu,
Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa habari za kifo cha Mtangazaji mkongwe, Julius Nyaisanga, maarufu kama Anko J.
Kwa wengi wetu, Julius Nyaisanga alikuwa ni zaidi ya Mtangazaji. Julius Nyaisanga alikuwa Mwalimu wetu.
Hapa nakumbuka kwa karibu kipindi chake cha maarifa miaka ile ya 70 mwishoni. Ilikuwa ni kwenye saa kumi na moja jioni. Julius Nyaisanga aliongoza mjadala wa wanafunzi waliotoka shule kadhaa za Sekondari. Kulikuwa na topics mezani na vijana wale walizichambua wakiongozwa na Julius Nyaisanga.
Katika miaka ya karibuni sijapata kushuhudia ubunifu na vipindi vyenye ubora kama ule. Vipindi vilivyotufanya hata sisi tuliokuwa Primary School enzi hizo kusogea kando ya redio na kuchota maarifa kutoka redioni.
Tutakukumbuka Anko J.
Maggid.
Iringa.
PICHA: Kwa Hisani ya Betty Mkwassa.

0 comments:

Post a Comment