Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha na Balozi wa Marekani nchini
Tanzania aliyemaliza muda wake Mhe Alfonso Lenhardt na mke wake leo
walipofika Ikulu kuaga na kumshukuru Rais na serikali yake kwa
ushirikiano aliowapa katika kipindi chao cha ubalozi hapa nchini.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimuaga mke wa Balozi wa Marekani nchini
Tanzania aliyemaliza muda wake Mhe Alfonso Lenhardt leo walipofika
Ikulu kuaga na kumshukuru Rais na serikali yake kwa ushirikiano aliowapa katika kipindi chao cha ubalozi hapa nchini. Mama Salma Kikwete alikuwepo pia katika kuwaaga wanadiplomasia hao.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza Balozi wa Marekani nchini Tanzania
aliyemaliza muda wake Mhe. Alfonso Lenhardt leo walipofika Ikulu
kuaga na kumshukuru.
(PICHA NA IKULU)
(PICHA NA IKULU)
---
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
BALOZI WA MAREKANI AMALIZA MUDA WAKE HAPA NCHINI
BALOZI WA MAREKANI AMALIZA MUDA WAKE HAPA NCHINI
Tanzania na Marekani zimeimarisha mahusiano
yao katika kipindi cha miaka minne iliyopita kutokana na uhusiano na
ushirikiano mzuri wa balozi anaemaliza muda wake nchini Mh. Alfonso
Lenhardt.
“Asante kwa kazi nzuri uliyoifanya katika
kipindi chote cha miaka minne uliyoitumikia hapa Tanzania. Mambo mengi
na makubwa yenye kuleta maendeleo na manufaa kwa Tanzania yamefanyika
hapa nchini na umeyasimamia na kuyafanikisha ipasavyo”.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemueleza
Balozi Lenhardt leo alipofika Ikulu kuaga na kumshukuru Rais na
serikali yake kwa ushirikiano alioupata katika kipindi chake cha ubalozi
hapa nchini.
Rais Kikwete amesema ushirikiano wa nchi
hizi mbili umekua na kuimarika zaidi na anatarajia kuwa balozi ajaye
naye atakuwa na mchango mkubwa katika kuendeleza na kuimarisha zaidi
mahusiano baina ya nchi hizi.
Naye balozi Lenhart amesema Tanzania iko moyoni mwake na ataendelea kuwa balozi wa Tanzania popote alipo.
“Nikushukuru wewe mheshimiwa Rais na
serikali yako kwa ushirikiano mzuri na utayari wa kunisikiliza na
kunisaidia wakati wote nilipohitaji ushauri wako, umekuwa msaada mkubwa
kwangu. Asante kwa ushirikiano wako na siku zote nitaendelea kuwa
balozi wa Tanzania kwani Tanzania iko moyoni mwangu”.
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu,
Dar es Salaam.
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu,
Dar es Salaam.
07 October, 2013
0 comments:
Post a Comment