Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akiwasili
Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es salaam jana kwa ajili ya
mazungumzo na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema kuhusu mkutano
wa hadhara wa kuhamasisha wananchi kuhusu mchakato wa katiba mpya,
utakaofanyika leo katika viwanja vya Jangwani
Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrajim Lipumba akiwasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia akiwasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi
Prof.
Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa habari kuhusu makubaliano
yao na Jeshi la Polisi kuhusu Mkutano wao utakaofanyika leo katika
viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam.
IGP, Said Mwema akizungumza na waandishi wa habari.
Karibuni
uwanja ni wenu, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema
akiwakaribisha viongozi wakuu wa vyama vitatu vya upinzani mbele ya
waandishi ya habari mara baada ya kumaliza mazungumzo yao ofisini
kwake.
IGP,
Said Mwema akiwashukuru viongozi wa vyama vya upinzani waliofika kwa
mazungumzo ofisini kwake. Kushoto ni Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim
Lipumba, mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mwenyekityi wa
NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba akipongezana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.
Picha Zote na Francis Dandee




0 comments:
Post a Comment