
DAKTARI anayedaiwa kuwa bandia amekamatwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, akiwa na vitambulisho bandia vya mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Muhimbili cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) akisomea Shahada ya Pili.
'Daktari' huyo ambaye amekuwa akitafutwa na uongozi wa chuo kwa zaidi ya mwaka alikamatwa jana asubuhi akiwa hospitalini hapo karibu na jengo kilimo kitengo cha meno.(P.T)
Katika kitambulisho chake cha kupigia
kura anatambulishwa kwa jina la Dismas John Macha aliyezaliwa mwaka 1979
Kilimanjaro na anaishi maeneo ya Upanga Magharibi, Dar es Salaam.
Gazeti hili, lilimshuhudia mtuhumiwa
huyo akiwa katika kituo cha usalama cha Muhas na kupekuliwa na askari
Polisi wa Muhimbili, Anthony Mwamatepela na kukutwa akiwa na vifaa vya
udaktari .
Baadhi ya vifaa alivyokutwa navyo ni
pamoja na koti jeupe la udaktari na stetoskopu ambacho ni kifaa cha
kusikilizia mapafu yanavyofanya kazi na mapigo ya moyo.
Pia alikuwa na begi jeusi lenye aina
mbalimbali za dawa, vitambulisho na karatasi nyingi, lakini alipoulizwa
alidai kuwa hizo ni dawa zake.
Macha alikutwa pia na vitambulisho
vitatu tofauti, kimoja kikimtambulisha kuwa mwanafunzi wa Muhas wa
Shahada ya Pili ya Udaktari (Masters of Medicine ) yenye jina la Macha
Dismas kikionesha kusajiliwa kwa namba 60520/2011 na kumaliza muda wake
Septemba 30 mwakani. Kitambulisho kingine kilimtambulisha kwa jina la
Macha Rogers anayesoma Shahada hiyo hiyo ikionesha kuwa anamaliza masomo
yake mwakani.
Alikutwa pia na kitambulisho
kinachomwonesha kuwa mwanafunzi wa Shahada ya Kwanza na kadi ya anuani
yenye jina la Amos Nnko ambaye ni Ofisa Rasilimaliwatu wa Chuo hicho.
Akizungumzia alivyomkamata askari wa
chuo hicho, Fulgence Semfukwe alisema walimkamata baada ya kupata
taarifa za yeye kuwa maeneo hayo na kupanga mbinu za kumkamata.
Alisema saa 4.45 asubuhi jana alimkuta
kwenye jengo la meno na kumwomba kwa nafasi yake ya udaktari amsaidie
tatizo lake na hivyo waongee pembeni, naye bila wasiwasi akakubali.
Alimwuliza anatibu magonjwa gani naye kumjibu anatibu maradhi ya aina
nyingi na kumwomba kitambulisho na yeye kumpa cha kwake.
Baada ya hapo alishituka na kudai kuwa
ni daktari wa Mwananyamala na amekuja hapo kwa ajili ya kuona wagonjwa
wake wa dharura ndipo alipokamatwa na kupelekwa kituo cha Polisi.
Alisema amekuwa akiwachenga kwa muda
mrefu kutokana na kuwa kila walipopewa taarifa yuko wodi au sehemu
Fulani hawakumkuta kwani walipishana naye baada ya kuvua koti na kuweka
kwenye begi lake jeusi.
Akizungumza na gazeti hili, Macha
limweleza mwandishi wa habari hizi kuwa yeye ni mwanafunzi ambaye
anaelewa masuala yote ya matibabu, lakini alifeli chuoni hapo mwaka
jana.
Alidai kuwa dawa alizokutwa nazo ni
zake kwani ana matatizo katika njia ya mkojo na kifua huku akiamua
kufanya hivyo kutokana na ugumu wa maisha.
"Uwezo wa kutibu ninao na nimesoma katika chuo hiki, lakini mwaka jana nilifeli ndiyo maana nikaamua kuwa hivi," alisema.
Ofisa Uhusiano wa Muhas, Hellen Mtui
alisema kutokana na kukamatwa na nyaraka akijitambulisha kuwa mwanafunzi
wa 'Masters of Medicine', ambaye anaweza kutibu watu hawana uhakika na
idadi ya watu ambao ameshatapeli hospitalini hapo.
Kuhusu kusoma Muhimbili, Mtui alikana
akisema baada ya kupekua nyaraka za chuo hawakubaini jina la mwanafunzi
wa aina hiyo na katika vyeti vyake bandia vinaonesha kusainiwa na Mkuu
wa Chuo aliyekuwapo kabla chuo hakijapanda hadhi na kuwa chuo kikuu.
Mtui alisema baada ya kumkamata na
kumpiga picha akiwa na mavazi ya udaktari, kumpekua na kumhoji
walimpeleka katika kituo cha Polisi cha Selander Bridge kwa mahojiano na
uchunguzi zaidi.
-Habari leo
Mjengwa Blog
Mjengwa Blog




0 comments:
Post a Comment