Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya HabariUtamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel, akizindua rasmi mbio zaRocky City Marathon 2013 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa UhusianoMwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Juma Kintu ambao wamedhamini mbio hizo kwa kutoa sh.milioni 15. (HM)
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Suleima Nyambui.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo nchini BMT, Dioniz Malinzi akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa mbio za Rocky Marathon.
MSIMU wa tano wa mbio za Rock City
Marathon umezinduliwa, ambapo mdhamini mkuu Shirika la Taifa la Hifadhi
ya Jamii (NSSF), limetaka kuwepo kwa mgawanyo wa majukumu kwa mbio za
umbali tofauti ili kuharakisha uendelezaji wa vipaji vya wanariadha
nchini.
Rock City Marathon zinaratibiwa na
Kampuni ya Capital Plus International (CPI), ambapo Ofisa Uhusiano wa
NSSF inayodhamini mbio hizo kwa mwaka wa nne sasa, Juma Kintu aliliomba
Shirikisho la Riadha Tanzania RT kugawana majukumu na wadau.
"Sisi kama NSSF tuko tayari kudhamini
na kuchangia maendeleo ya riadha nchini, ndio maana tunasisitiza mgao wa
majukumu kwa wakimbiaji wa umbali fulani kusimamiwa na taasisi au
kampuni moja, ili kusaidia maendeleo ya haraka na makuzi sahihi ya
vipaji," alisema Kintu.
Pamoja na NSSF, wadhamini wengine wa
Rock City Marathon 2013 zitakazofanyika jijini Mwanza Oktoba 27 ni
pamoja na PPF, Airtel, African Barrick, Nyanza Bottlers, Sahara Media,
Precission Air, Bank M, New Mwanza
Hotel na Umoja.
Hotel na Umoja.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante
Ole Gabriel, aliyekuwa mgeni rasmi, alisema mchezo wa riadha nchini
unaelekea kuangamia na jitihada za
kuunusuru zinahitajika.
kuunusuru zinahitajika.
"Ni aibu kuwa mchezo wa riadha nchini
unaelekea kufa wakati viongozi waliopewa mamlaka ya kuhakikisha
unaendelea wanashuhudia. Ni wakati wa kuamka kuunusuru mchezo huu ambao
katika miaka ya 1970 mpaka 1980 uliiletea nchi yetu heshima kubwa.
Kwa upande wake, Rais wa RT, Suleiman
Nyambui aliwataka waratibu wa marathon kote chini kuhakikisha wanakuwa
na mbio fupi za vijana ili kupanua wigo wa kuzalisha vipaji vipya,
vitakavyoliletea sifa taifa na kushinda mashindano mbalimbali ya kitaifa
na kimataifa.
Naye Mgurugenzi Mtendaji wa Capital
Plus, Ellen Otaru Okoedion, aliishukuru Serikali kwa ahadi ya
ushirikiano, lakini akaitaka kuhakikisha inakaa mezani na (kina Nyambui)
RT, ili kujadili njia sahihi zitakazofanikisha kupatikana kwa kina
'Nyambui wapya.'
Aidha, Mratibu wa tukio hilo, Mathew
Kasonta alisema kuwa mbio hizo zitajumuisha kilometa tano kwa wakimbiaji
kutoka katika makampuni, kilometa tatu kwa wenye ulemavu, kilometa tatu
kwa watu wazima (zaidi ya miaka 55) na kilometa mbili kwa watoto wenye
umri kati ya miaka 7 mpaka 10.
Chanzo: fullshangwe
0 comments:
Post a Comment