SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, September 19, 2013

Wananchi zaidi ya 200 Mvomero wavamia na kugawana heka 500 za mwekezaji.

Zaidi ya wananchi 200 wa kijiji cha kibaoni wilayani mvomero mkoani morogoro hawana maeneo ya kulima baada ya serikali ya kijiji hicho kuuza maeneo ya mashamba zaidi ya ekari 500 kwa mwekezaji huku wananchi hao wakitishia kuandamana na kujichukulia sheria mkononi ya kuvamia na kugawana maeneo ya mashamba hayo Wakizungumza wakati wakigawana mashamba hayo 
wananchi hao wamesema kuwa wamegawana mashamba kwa wananchi wote ambapo kila mwananchi amepata ekari mbili na kusema wanashangaa kuona mipaka inawekwa katika maeneo yao kuashiria kuuzwa kwa eneo hilo bila taarifa huku wakiendelea kukosa maeneo kwa ajili ya shughuli za kilimo hali inayopelekea kushindwa kulea familia zao.

 Naye afisa mtendaji wa kijiji cha Kibaoni Lucas Kiwele amekiri kuwepo kwa mgogoro huo na kudai kuwa eneo hilo linamilikiwa na serikali ya kijiji na kwamba serikali ya kijiji haikuhusika kuuza eneo hilo na liliuzwa na wananchi wenyewe ambapo amewataka wananchi kufuata sheria na taratibu za ardhi katika ugawaji wa mashamba...lucas kiwele afisa mtendaji kijiji cha kibaoni

0 comments:

Post a Comment