SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, September 9, 2013

UWSA yanasa nyumba inayofanya wizi wa maji eneo la Chekereni.

 Maofisa wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi(MUWSA)wakifukua sehemu inayodaiwa kuunganishwa maji kinyemela kwenda katika moja ya nyumba ambayo haikuwahi kuunganishiwa maji na mamlaka hiyo.
Maji yanatoka kwa wingi hapa
 Moja ya tanki la maji la chini linalokadiliwa kuwa na ujazo wa lita 10000 ambalo limekua likitumika kuajaza maji yaliyounganishwa katika mtandao wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi,(MUWSA).
 Maofisa wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi(MUWSA)waakiongozwa na ofisa uhusiano wa mamlaka hiyo Dorah Killo wakiangalia kinachodaiwa kuwa ni hujuma ya maji iliyofanywa na mmiliki wa nyumba moja katika eneo la Chekereni weruweru.
Mojawapo ya matanki
 Moja ya mashine maalumu ya kupandishia maji katika tanki la juu lenye ujazo wa lita 2000 lilipo kwenye eneo la nyumba ambayo inadaiwa kufanya hujuma kwa kuiba maji ya mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi(MUWSA)
 Nyumba ambako inadaiwa kufanyika wizi wa maji ya mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi unafanyika.
 Ofisa uhusiano wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi akizungumza na mwenyekiti wa kitongoji cha Katanini katika kijiji cha Chekereni weruweru Yahaya Salum kuhusiana na tukio hilo la kinachodaiwa kuwa ni hujuma ya wizi wa maji katika nyumba hiyo.
 Sehemu ambako wizi wa maji unadaiwa kufanywa na mmiliki wa nyumba hiyo.
Fundi wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi akijaribu kufungua sehemu ya maungio ambako inadaiwa wizi wa maji umekuwa ukifanyika. Picha na Dixon Busagaga, Globu ya Jamii, Moshi
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi. 
 MAMLAKA ya maji safi na maji taka mjini Moshi(MUWSA) imefanikiwa kunasa moja ya nyumba ya kisasa iliyopo eneo la Chekereni Weruweru ambayo mmiliki wake anadaiwa kujiunganishia maji kinyume cha sheria.
Mbali na wizi huo pia Kigogo huyo amejenga tanki la maji la chini linalokadiriwa kuwa na ujazo wa lita 10000 za maji lingine dogo lenye ujazo wa lita 2000 ambalo pembeni yake imejengewa mashine maalumu ambayo imekuwa ikitumika kupandisha maji.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi,MUWSA na kuthibitidhwa na ofisa habari wake Dorah Killo zilionesha mmiliki huyo hakuwahi kuunganishiwa maji katika nyumba yake hiyo ambayo pia imetia shaka katika ujengwaji wake hadi kukamilika. “Kwa sasa tunashindwa kutoa taarifa za huyu mmiliki wa nyumba hii kwa sababu hatuna taarifa zake ofisini ingawaje zipo taarifa zisizo rasmi kuwa ni mkaguzi wa mahesabu na kama ulivyoona amejiunganishia maji pasipo kufuata utaratibu, hiii ni hujuma kwa mamlaka lakini pia ni hujuma kwa serikali…tutamchukulia hatua mtu huyu zinazomstahili”alisema Killo. 
 "Kumekuwepo na upotevu mkubwa wa maji katika kijiji hiki, kwani kwa siku tumekuwa tukizalisha maji mita za ujazo 1,200, lakini asilimia 80 ya maji hayo hupotea, na upotevu huu husababishwa na watu kujiunganishia maji kinyume cha sheria," aliongeza Killo. 
 Alifafanua kuwa Mamlaka hiyo kwa sasa hupoteza asilimia 28 ya maji yanayozalishwa ambapo asilimia 80 ya upotevu wa maji kati ya hizo inatoka katika kijiji cha Chekereni Weruweru. 
 Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Serikali ya Kitongoji cha Katanini katika kijiji cha Chekereni Weruweru, Yahaya Salum,alikiri kufuatwa na maofisa wa Muwsa na kuonyeshwa namna mkazi wa kitongoji hicho alivyojiunganishia maji kinyume cha sheria na kuwaomba wananchi kuacha mara moja wizi huo.
NA MICHUZI MATUKIO

0 comments:

Post a Comment