
Wauguzi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga wakimuhudumia hakimu Satto
Nyangoha aliyechomwa kisu shavuni jana, akiwa mahakamani na mlalamikaji
katika kesi ya wizi wa baiskeli, Emmanuel Izengo. Picha na Suzy Butondo
====
Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo iliyopo eneo la Nguzo Nane, Kata
ya Kambarage Mjini Shinyanga, Satto Nyangoha amejeruhiwa kwa kuchomwa
kisu katika shavu lake la kushoto baada ya kutoa hukumu ya kesi ya wizi
wa baiskeli.
Kitendo hicho kinadaiwa kufanywa na mlalamikaji
katika kesi hiyo, Emmanuel Izengo (28), mkazi wa Tambukareli, Shinyanga
baada ya kutokuridhishwa na hukumu iliyotolewa bila ya mshtakiwa, Daniel
Makelezia, mkazi wa Lubaga Shinyanga na mdhamini wake, Marko Nkelezia
kuwepo mahakamani.
Katika hukumu yake, Hakimu Nyangoha alisema
mshtakiwa atakapopatikana atatumikia kifungo cha miaka miwili jela baada
ya kupatikana na hatia ya wizi wa baiskeli hiyo aina ya Neria yenye
thamani ya Sh150,000.
KWA HABARI ZAIDI




0 comments:
Post a Comment