
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Vifaa vya Mtandao wa Teknolojia ya Kisasa ya Zhong Xing Telecommunication Equipment { ZTE }ya Nchini China Bwana Chen Jinsong akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa ZXanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Kulia yao ni Mwakilishi wa Kampuni hiyo Nchini Tanzania ambayo ndio inayosimamia ujenzi wa Mkongo wa Taifa Zanzibar Bwanan Wayne Zhu.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akibadilishana mawazo na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Vifaa vya Mtandao wa Teknolojia ya Kisasa ya Zhong Xing Telecommunication Equipment { ZTE } ya Nchini China Bwana Chen Jinsong.

Mwenyekiti wa Kampuni inayoendesha Miradi ya Hoteli za Kimataifa Afrika Mashariki iitwayo Mada Hotels yenye Makao Makuu yake Mjini Nairobi Nchini Kenya Bwana Tinu Mhajan akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akielezea fursa za uwekezaji zilizopo Zanzibar katika sekta ya Utalii mbele ya Mwenyekiti wa Kampuni inayoendesha Miradi ya Hoteli za Kimataifa Afrika Mashariki iitwayo Mada Hotels yenye Makao Makuu yake Mjini Nairobi Nchini Kenya Bwana Tinu Mhajan
Mwenyekiti huyo wa Mada Hotels alifika Zanzibar kuangalia maeneo ambayo Kampuni yake inaweza kuwekeza katika ujenzi wa Hoteli za Kitalii.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Na Othman Khamis Ame, OMPR
Uchumi wa Mataifa machanga yanayolenga kuelekea kwenye maendeleo ya haraka utazidi kuimarika iwapo Mataifa hayo yatajikita zaidi katika matumizi ya Mfumo wa Teknolojia ya Kisasa ya Mawasiliano ya moja kwa moja kati yao au hata kushirikiana pamoja na yale Mataifa yaliyoendelea.
Hayo yaliibuka wakati wa mazungumzo kati ya Ujumbe wa Kampuni ya Vifaa vya Teknolojia ya Mawasiliano { Zhong Xing Telecommunication Equipment } {ZTE } yenye Makao Makuu yake Nchini China ulioongozwa na Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo Bwana Chen Jinsong pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Bwana Chen Jinsong ambae Kampuni yake ya ZTE ndiyo inayojenga na kusimamia mradi wa Mkongo wa Taifa hapa Zanzibar alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kuwa mfumo huu wa mawasiliano hutoa fursa kwa wataalamu wa pande mbili walio Nchi tofauti kufanya kazi pamoja kwa kutumia mtandao wa kisasa wa mawasiliano ya Teknolojia.
Alifahamisha kwamba hatua za Kiuchumi , Biashara, Afya pamoja na harakati za maisha ya Jamii za kila siku zina nafasi na fursa nzuri ya kutumia Mtandao wa Serikali { E. Government } wakati utakapokamilika matengenezo yake Mfumo huo.




0 comments:
Post a Comment