Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif,
akisalimiana na Wanavikundi vya Ushirika wa Wanaweke Mkoani Pemba
akiongoza ziara ya Wake wa Wawakilishi na Wbunge kutembelea Vikundi vya
Wanawake na kutowa misaada katika vikundi hivyo.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif,
akimkabidhi mmoja wa Wanavikundi vya Ushirika vya Mkoani fedha taslim
Shilingi laki nne, kwa ajili ya kuendelea vikundi hivyo vya
Kinamama,Fedha hizo zimetolewa na Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, Mke wa Makamu wa Pili wa
Rais Mama Asha Balozi Seif na Wake wa Wawakilishi na Wabunge wa CCM,
jumla ya Vikundi Sita vimefaidika na msaada huo katika Wilaya ya
Mkoani Pemba.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif,
akimkabidhi Mwanachama wa Kikundi cha Tuishi kwa Usalama cha Mkoani Tatu
Mohammed Ussi, mkopo wa shilingi laki tano uliotolewa na kikundi hicho
kwa Mwanachama wake. wakati wa ziara ya Umoja wa Wake wa Viongozi
waCCM, Wilaya ya Mkoani Pemba.
Wanavikundi vya Ushirika wa Wanawake Wilaya ya Mkoani wakimsikiliza Mke
wa Makamu wa Pili swa Rais wa Zanzibar akitowa nasaha zake kwa
Wanaushirika hao, katika ukumbi wa Umoja ni Nguvu.
MKE wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, Mjumbe
wa Kamati Kuu ya Taifa Maua Daftari na Bihindi Hamad wakisikiliza risala
ya Wanaushirika.wakati wa kutowa misaada kwa Vikundi vyao katika ukumbi
wa Umoja ni Nguvu Mkoani.
WANAUSHIRIKA wakishangilia katika mkutano wa kukabidhi misaada
iliotolewa na Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein na Umoja wa Wake wa Wawakilishi na
Wabunge kwa vikundi hivyo.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi akitembelea
vikundi vya Ushirika vya Wanawake wa Wilaya ya Mkoani , baada ya
kukabidhi michango yao kwa Vikundi hivyo katika Ukumbi wa Umoja ni Nguvu
Mkoani.kuangalia bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na Vikundi hivyo.
CHANZO: ZANZINEWS
CHANZO: ZANZINEWS
0 comments:
Post a Comment