Mkurugenzi wa MISA-TAN Bw. Tumaini Mwailenge akizungumza na waalikwa kwenye Gala Dinner ya kuadhimisha siku ya Uhuru wa habari Duniani iliyoenda sambamba na uzinduzi wa Mfuko wa Mwangosi utakao kuwa ukisaidia waandishi wa habari pindi wapatapo matatizo wakiwa kazini. Kushoto ni Mzee Kassim Mapili wa Mjomba waliosherehesha usiku huo kwa buradani ya aina yake.(Picha na Dewji Blog).
Baadhi ya Wanahabari walioshiriki kwenye Gala Dinner ya siku ya Uhuru wa Habari iliyoenda sambamba na Uzinduzi wa Mfuko wa Mwangosi kusaidia waandishi wa habari ambao wamepata matatizo wakiwa kazini.
Blogger Pamela Mollel (katikati) wa Jamii Blog ya jijini Arusha akibadilishana wanahabari wenzake Tonia Kasoni( kushoto) wa Radio 5 pamoja na Mhariri wa Sibuka TV wakati wa hafla hiyo.
Mjane wa Marehemu Daudi Mwangosi na mtoto wa mwisho wa marehemu wakati wa uzinduzi wa Mwangosi Fund utakaokuwa ukisaidia waandishi wa habari wanaopata majanga wakiwa kazini vile vile utaenda sambamba na Tuzo ya Mwandishi ambaye atakuwa amepata matatizo, misukosuko katika kutafuta habari za uchunguzi na Tuzo hiyo itakuwa ikitolewa kila mwaka Septemba 6 siku aliyokufa Daudi Mwangosi na mshindi wa Tuzo hizo atajinyakulia Milioni 10 zitakazotolewa na waendeshaji wa mfuko huu UTPC.
Mzee Kassim Mapili wa Mjomba Band akikung'uta gitaa wakati akipiga wimbo wa Mbaraka Mwishe" Njoo mjionee Morogoro"....wakati wa hafla ya kuchangisha fedha za mfuko wa Daudi Mwangosi zilizoenda sambamba na uzinduzi wa mfuko huo katika hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha.
Mmoja wa waandishi wa siku nyingi kwenye tasnia ya habari ambaye pia ni Mwanaharakati wa kutetea haki za Wanawake Bi. Leila Sheikh akiimba nyimbo za zamani pamoja na Mjomba Band inayoongozwa na Mzee Kassim Mapili na Mrisho Mpoto.
Bi. Leila Sheikh akisakata Rhumba la enzi hizo sambamba na Mzee Makwaiya Wakuhenga wakati Gala Dinner katika kuadhimisha siku ya Uhuru wa Habari Duniani kwenye Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha usiku wa kuamkia leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Abubakar Karsan.
Wanahabari kutoka Zanzibar nao walijumika na wenzao wa Bara kutoka nchini za Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Gala Dinner.
Wakongwe katika tasnia ya habari hapa nchini akiwemo Mzee Salim Salim na Mzee Hamza Kasongo na wenzao wakibadilishana mawazo.
Mgeni rasmi kwenye Gala Dinner ya kuadhimisha siku ya Uhuru wa Habari duniani ulioenda sambamba na uzinduzi wa Kitabu kilichoandaliwa na Media Council Tanzania (MCT) pamoja na Kitabu cha Uhuru wa Vyombo vya Habari Kusini mwa Jangwa la Afrika Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Assah Mwambene akitoa salamu za Rais Kikwete za Pongezi kwa wanahabari Tanzania kwa kuadhimisha siku ya Uhuru wa Habari Duniani ambapo Serikali imeahidi kushirikiana na wanahabari bega kwa bega kwa mustakabali wa kuboresha tasnia hiyo.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Assah Mwambene akizindua Ripoti ya Habari hapa nchini ya mwaka 2012 iliyoandaliwa na Media Council of Tanzania (MCT) aliyeshika kitabu hicho ni Afisa Mipango Mwandamizi wa Taasisi ya Media Council of Tanzania (MCT) Bi. Alakok Mayombo na Mjumbe wa MCT Bw. Allan Lawa na MC wa Gala Dinner hiyo Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania Jane Mihanji.
Sasa imezinduliwa rasmi.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Assah Mwambene, Mwenyekiti wa Misa-Tan Bw. Mohammed Tibanyendera na mwakilishi wa Ubalozi wa Ireland kwa pamoja wakizuindua Kitabu cha Uhuru wa Vyombo vya Habari Kusini mwa Jangwa la Afrika kilichoandaliwa na MISA katika Gala Dinner ya kuadhimisha siku ya Uhuru wa Habari Duniani.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Assah Mwambene akionyesha kitabu "SO THIS IS DEMOCRACY" mara baada ya kukizindua rasmi.
Usia Nkhoma wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na mwanahabari mwenzake wakifurahia jambo wakati wa hafla hiyo.
Mzee Hamza Kasongo akiendesha Harambee kwa wanahabari na wahariri kwa ajili ya kuchangisha mfuko wa Mwangosi utakaokuwa ukisaidia wanahabari pindi wapatapo matatizo kazini.
Stella Vuzo wa UNIC akitangaza ahadi yake binafsi ambapo ameahidi kutoa Dola 300 kuchangia Mfuko wa Mwangosi.
Mwenyekiti wa Misa-Tan Bw. Mohammed Tibanyendera akitoa ahadi yake binafsi ambapo ameahidi kuchangia Laki moja huku Misa-Tan imetoa ahadi ya Shilingi Milioni moja kuchangia mfuko wa Mwangosi uliozinduliwa rasmi usiku wa kuamkia leo katika Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha.
Mwakilishi kutoka BBC ambao nao pia waliguswa na kuchangia mfuko wa Mwangosi kiasi cha Shilingi Milioni Mbili.
Mwendeshaji wa Harambee hiyo Mzee Hamza Kasongo akitangaza kiasi cha fedha zilizokusanywa kwenye Harambee hiyo ambacho ni zaidi ya shilingi Milioni 19 wakati wa Gala Dinner ya kuadhimisha siku ya Uhuru wa Habari duniani.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Assah Mwambene akikabidhi fedha taslim shilingi laki 5 zilizokusanywa kwenye Harambee hiyo kwa Rais wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Kenneth Simbaya.
CHANZO: BOFYA HAPA
CHANZO: BOFYA HAPA
0 comments:
Post a Comment