SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, May 17, 2013

Mke wa waziri Mkuu pinda afungua kongamano la Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA) jijini Arusha Jana.

Mgeni rasmi Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda (wa tano kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi viongozi wakuu wa TAPSEA pamoja na waratibu wa Kongamano hilo la Makatibu Muhtasi  Tanzania lililofanyika Jana kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa  jijini Arusha-AICC.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Uwezeshaji na Uwekezaji,ambaye pia ni mlezi wa TAPSEA.Dkt Mary Naguakimkabidhi zawadi ya kinyago mgeni rasmi,Mke wa Waziri Mkuu,Mh.Mama Tunu Pinda ,shoto kwake ni Mwenyekiti wa TAPSEA,Bibi Pili Mpenda wakati wa Kongamano la tatu la Makatibu Muhtasi Tanzania.
Mgeni rasmi,Mke wa Waziri Mkuu,Mh.Mama Tunu Pinda akifungua Kongamano la tatu la Makatibu Muhtasi Tanzania,lililofanyika kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa  jijini Arusha-AICC ..
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Uwezeshaji na Uwekezaji,ambaye pia ni mlezi wa TAPSEA.Dkt Mary Nagu akizungumza jambo mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye kongamano tatu la Makatibu Muhtasi Tanzania,lililofanyika kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa  jijini Arusha-AICC .

Waziri wa  Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,Mh.Sofia Simba akizungumza jambo mbele ya wageni waalikwa mbalimbali kwenye
mkutano wa Kongamano  la  tatu la Makatibu Muhtasi  Tanzania,uliofanyika mapema leo  kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa  jijini Arusha-AICC .
Sehemu ya meza kuu ndani ya mkutano wa kongamano la tatu la Makatibu Muhtasi  Tanzania lililofanyika Jana kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa  jijini Arusha-AICC,kutoka kushoto ni  Waziri wa  Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,Mh.Sofia Simba,Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Uwezeshaji na Uwekezaji,ambaye pia ni mlezi wa TAPSEA.Dkt Mary Nagu,Mgeni rasmi wa Kongamano hilo la TAPSEA,Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda,Mwenyekiti wa TAPSEA,Bibi Pili Mpenda pamoja naNaibu Waziri wa katiba na sheria ambaye pia ni Mshauri wa masuala ya sheria na kazi waTAPSEA,Bi.Angella Kairuki.
Pichani ni sehemu ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye kongamano la tatu la Makatibu Muhtasi  Tanzania lililofanyika Jana kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa  jijini Arusha-AICC. 
Pichani juu ni sehemu ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye kongamano la tatu la Makatibu Muhtasi  Tanzania lililofanyika Jana kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa  jijini Arusha-AICC.
Baadhi ya wageni waalikwa kutoka sehemu mbalimbali wakijiandikisha tayari kwa kushiriki kwenye kongamano la tatu la Makatibu Muhtasi  Tanzania lililofanyika leo kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa  jijini Arusha-AICC.
Mwenyekiti wa TAPSEA,Bibi Pili Mpenda akimkaribisha mmoja wa wageni maalum wa kongamano hilo,Naibu Waziri wa katiba na sheria ambaye pia ni Mshauri wa masuala ya sheria na kazi waTAPSEA,Bi.Angella Kairuki alipokuwa akiwasili kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa  jijini Arusha-AICC .
Mwenyekiti wa TAPSEA,Bibi Pili Mpenda akimkaribisha Mgeni rasmi,Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda alipokuwa akiwasili mapema Jana kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa  jijini Arusha-AICC .
Wakielekea kwenye  ukumbi wa mikutano ambao Kongamano la  kwenye kituo cha mikutano cha kongamano la tatu la Makatibu Muhtasi  Tanzania (TAPSEA), lililofanyika leo kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa  jijini Arusha-AICC .

Mgeni rasmi,Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda  (wa pili kushoto) pamoja na wageni waalikwa wengine wakitazama ngoma ya kimasai iliyokuwa ikitumbuiza nje ya jengo la mikutano la AICC kabla ya mkutano wa Kongamano  la  tatu la Makatibu Muhtasi  Tanzania kuanza.
PICHA, HABARI NA MICHUZI MATUKIO BLOG

0 comments:

Post a Comment