SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, May 17, 2013

Bajeti ya Wizara ya Viwanda na Biashara yapita.

Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda akisoma hotuba ya Wizara yake Bungeni, jumatano wiki hii.
 
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda na Naibu wake Mh Gregory Teu wakisikiliza kwa makini michango ya Wabunge kwa Wizara yao. Watumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo wakifuatilia mawasilisho ya bajeti yao Bungeni mjini Dodoma. Wataalamu wa Wizara ya Viwanda na Biashara wakitayarisha majibu ya hoja na michango mbali mbali ya Wabunge iliyoelekezwa kwa Wizara hiyo.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda na Naibu wake Mh Gregory Teu wakibadilishana mawazo na Mbunge Sanya nje ya ukumbi wa Bunge.
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akiwaongoza Mawaziri na Naibu Mawaziri kuwapongeza Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda na Naibu wake Mh Gregory  Teu baada ya  Bunge kupitisha bajeti ya Wizara hiyo.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda na Naibu wake Mh Gregory Teu wakipongezwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi Joyce Mapunjo nje ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya Bajeti ya Wizara hiyo kupitishwa na Bunge.Watumishi na Viongozi wa Wizara ya Viwanda na Biashara wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya ukumbi wa Bunge baada ya Bajeti yao kupita.
NA DEWJI BLOG

0 comments:

Post a Comment