Siku ya Jumamosi tarehe 27.10.12 Mh Balozi wetu wa Tanzania nchini Uingereza,Mh. Peter Kallaghe alishiriki sherehe ya siku kuu ya Iddi iliyofanyika London mashariki.
****
Sherehe hii ya baraza la EID (IDDI) iliyoandaliwa na Jumuiya ya East African Education Foundation wakishirikiana na Jumuiya ya Wazanzibari waishio UK (ZAWA).
Wakati akitoa hotuba yake Mh Balozi Peter Kallaghe ambaye ndio aliekua mgeni rasmi siku hiyo, alianza kwa kuwashukuru kwa mualiko huo mzuri alioupata na kuwatakia kila kheri wale wote waliofanikiwa kutekeleza HIJA kwa mwaka huu 2012.
Aidha Mh Balozi aliahidi kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya Ubalozi na Jumuiya mbalimbali za Watanzania zilizopo nchini Uingereza na Ireland.
Pia alivutiwa na kuipongeza hatma ya East African Education Foundation kuazimia kununua Jengo kwa ajili ya shughuli za kijamii na wanajumuiya wote kwa ujumla. Baada ya kumaliza hotuba yake Shekhe Nasssor Haroub nae aliongea na wanajumuiya akitilia mkazo zaidi umuhimu wa Umoja na mshikamano kama Uislamu unavyo sisitiza kupitia Ibada ya HIJA.
Vilevile vijana wa kasida walipata fursa ya kutumbuiza alipomaliza kuongea Shekhe Nassor. Mwishoni Balozi alifanya ziara fupi ya kukagua jengo la Jumuiya hiyo na kupata maelezo kutoka kwa viongozi mbalimbali wa Jumuiya ili kujua namna gani litakavyoweza kutumika mara baada ya hatua za ununuzi zitakapo kamilika rasmi kwa gharama za paundi laki 6 (£600,000)
Asanteni,
Urban Pulse Creative
Mh Balozi katika akipokea zawadi kutoka kwa wanajumuiya
Mh. Balozi Peter Kallaghe akiwa katika Picha ya pamoja na Wanajumuiya ya East African Education Foundation.
Mwenyekiti wa ZAWA,Hassan Khamis akimfafanulia jambo Mh Balozi.
Ustadhi akiongea machache wakati wa chakula.
Vijana wa Kasida wakitumbuiza.
watoto wa Kasida wakisikiliza Hotuba ya Mh Balozi.
0 comments:
Post a Comment