TOKA WAVUTI: Yatokanayo na msiba wa Domi: Funzo kwa wanaoishi ndani na nje ya Tanzania
Hii ni rekodi kutoka kwenye kipindi cha "Weekend Special" cha redio WAPO FM kuhusu yaliyotokea baada ya msiba wa Domi ambapo familia ya marehemu ilirusha madai kuhusu mali na fedha na kuweka zuio kwamba mke asiruhusiwe kusafiri kutoka Tanzania kurudi Marekani waliko watoto wake.
Mtangazaji wa WAPO Radio, Anthony Joseph, alizungumza na kila upande unaohusika na suala hili na kisha kuzikutanisha pamoja ili kuwekana sawa kuhusu tuhuma zilizotamkwa.
Dada Subi wa blogu ya WAVUTI aliweza kukisikiliza kipindi hiki na kukirekodi kwa maombi maalum na kisha kuiweka HAPA Kwa mujibu wa Dada Subi, anasema "baada ya kukisikiliza, nimejifunza mengi ambayo ningependa na wengine wajifunze na kuchukua hatua madhubuti. Changamoto za maisha ya ndoa, ughaibuni, familia na tamaduni mbili zilizo mbalimbali!"
NINALOWEZA KUSEMA NI KUWA...SIKILIZA NA TAFAKARI
SOURCE:BOFYA HAPA
0 comments:
Post a Comment