SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, July 27, 2012

Chuo Kikuu chapoteza Wanafunzi 14 ajali ya Mv Skagit

 Mv Skagit
Chuo Kikuu cha Waislamu kilichoko mkoani Morogoro kimepoteza wanafunzi 14 wa mwaka wa kwanza katika ajali ya boti ya Mv Skagit iliyotokea Julai 18, mwaka huu katika Bahari ya Hindi karibu na kisiwa cha Chumbe.

Waliofariki na sehemu wnazotoka katika mabano ni Abdalla Mohamed wa Unguja; Suleimani Ally (Pemba); Othumani Mwinyi Hussein (Unguja); Rashid Salehe (Unguja); Rashidi Juma (Pemba); Hussan Seif (Unguja); Mangi Haji (Unguja); Asha Abdalla (Pemba); Said Iddi (Unguja); Khadija Khamis (Pemba); Mgeni Omari (Unguja); Patima Simai (Unguja); Said Khatib (Pemba) na Khamis Suleimani (Unguja).

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Ofisa Habari wa chuo hicho, Saddy Ally, ilisema miili ya wanafunzi 12 ilipatikana na kuzikwa na miwili haijapatikana.



Alisema kuwa msiba huo ni mkubwa na pigo kubwa kwa chuo hicho na kwa Taifa kwa ujumla.

Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Hamza Njozi, aliwapa pole wale wote waliofikwa na msiba huo na kuwaomba ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza ndugu zao katika ajali hiyo kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu.

Aidha, Profesa Njozi alisema ni jambo la kusikitisha sana kwani chuo kimepoteza wanafunzi wengi ambao walikuwa ni wa mwaka wa kwanza licha ya kwamba pia katika ajali ya Mv Spice iliyotokea mwaka jana wanafunzi wawili wa chuo hicho waliopoteza maisha.

0 comments:

Post a Comment