SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, June 1, 2012

AIRTEL YATOA BURUDANI KWA KUDHAMINI ONESHO LA MUZIKI WA CLASSIC


Kikundi cha muziki wa taratibu (classic) cha Dar Choral Society kikitoa burudani katika onyesho la muziki huo lililodhaminiwa na Airtel katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam jana.

Meneja Huduma wa Airtel, Hilda Nakajumo akitoa maelezo kwa Mkuu wa Biashara wa Benki ya Africa, Wasia Mushi kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Airtel katika onyesho kikundi cha Dar Choral Society lililodhaminiwa na Airtel katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam jana.


Baadhi ya waimbaji wa kikundi cha Dar Choral Society wakiimba katika onyesho la lililodhaminiwa na Airtel katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam jana.

Baadhi ya watu wakiohudhuria onyesho hilo wakipata maelezo ya huduma zitolewazo na Airtel katika eneo lililowekwa ambapo huduma mbalimbali zilipatikana.

Baadhi ya wanamuziki wa Dar Choral Society wakiwa kazini katika onyesho lililodhaminiwa na Airtel katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Mtaa wa Shaaban Robert, Dar es Salaam jana.

Baadhi ya watu waliohudhuria onyesho la kikundi cha muziki cha Dar Choral Society wakishangilia katika onyesho hilo lililodhaminiwa na Airtel katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Dar es Salaam jana.

Mkurugenzi wa Biashara wa Airtel Tanzania, Irene Madeje Mlola
(kushoto) akizungumza na baadhi ya watu waliohudhuria onyesho la kikundi cha muziki cha Dar Choral Society lililodhaminiwa na Airtel katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Dar es Salaam jana.

0 comments:

Post a Comment