SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, February 16, 2012

WANUSURIKA KATIKA AJALI YA BASI MBEYA

Basi la Happy Nation limeanguka baada ya kushindwa kuumudu mteremko wa TAZAMA, maarufu kama Pipeline. Habari toka kwa abiria waliopanda basi la Nganga, anasema watu wamejeruhiwa vibaya ila hakuna vifo. Basi hilo likiwa kwenye mwendo kasi lilitaka kulipita basi la Nganga, lakini kukawa na gari jingine linapandisha mlima huo, ndipo dereva akalazimika kulirudisha nyuma ya basi la Nganga na kuligonga kwa nyuma na kupinduka. Abiria wa basi la Nganga wamesalimika wote.
Picha na Felix Mwakyembe.

0 comments:

Post a Comment